Rayvanny na Marioo kuachia kibao cha pamoja

Muhtasari

• Huenda mashabiki wa muziki wakashuhudia kolabo nyingine kati ya Rayvanny na Marioo .

• Hili linajiri baada ya Rayvanny kupakia video katik ukurasa wake wa Instagram ikionyesha wawili hao wakiwa studio, katika shughuli rasmi ya kuandaa muziki mpya.

Instagram KWA HISANI
Instagram KWA HISANI
Image: Marioo na Rayvanny

Huenda mashabiki wa muziki wakashuhudia kolabo nyingine kati ya Rayvanny na Marioo .

Hili linajiri baada ya Rayvanny kupakia video katik ukurasa wake wa Instagram ikionyesha wawili hao wakiwa studio, katika shughuli rasmi ya kuandaa muziki mpya.

Ifahamike kwamba kibao cha mwisho ambacho Chui alimshirikisha Marioo kilikuwa TeQuiero ambacho kilifanya vizuri katika chati za muziki ndani ya bongo na Afrika Mashariki.

Kutokana na video hiyo ya Rayvanny, huenda wazalishaji  [producer] S2kizzy na Soundboy wakahusika katika kuandaa kibao hicho.

Kibao hicho kinatarajiwa kuachiliwa wakati ambapo Marioo anazidi kufanya vizuri kimuziki kwa nyimbo zake ambazo zimetokea kupendwa na mashabiki wengi.

Kwa upande wake Rayvanny amehusishwa na  kuondoka WCB ila alishikilia kwamba wakati ukifika ataondoka bila vurugu yoyote.

Kwa sasa mashabiki watalazimika kusubiria kazi hiyo kutoka kwa magwiji hao wawili.