"Kaa mbali na maisha yangu, mimi sio kama mbwa wako," Baba Levo ampasha Shilole

Muhtasari

• "Kuanzia Leo Kaa Mbali Na Maisha Yangu Mi Sio Hao Mbwa Wako Unaowafuga Nakujua Vyema Usitake Niongee Tafadhali" - Baba Levo kwa Shilole

Baba Levo na Shilole
Baba Levo na Shilole
Image: Screengrabs

Kuna timbwiri lilaloendelea baina ya msanii Baba Levo na msanii wa kike Shilole na inaonekana imekula kwa Baba Levo ambaye ndiye ameonekana kukerwa zaidi ya kuamua kumwaga ubuyu.

Baba Levo ameingia kwenye Instagram yake na kumpa msomo wa karne msanii Shilole huku akimtaka akae mbali kabisa na maisha yake kama vile magharibi iko mbali na mashariki.

Wengi wanamjua Baba Levo kwa utata wake wa kuzungumza mambo jinsi yalivyo bila kutetereka wala kuwa na fikira ya akiba.

“Kuanzia Leo Kaa Mbali Na Maisha Yangu Mi Sio Hao Mbwa Wako Unaowafuga Nakujua Vyema Usitake Niongee Tafadhali,” Baba Levo alimkemea Shilole kupitia kwa instastories zake huku akiandika maandishi haya juu ya picha ya Shilole.

Baadhi ya watu waandhani ni mzaha tu wa kukurupukiana kwa maneno mitandaoni kutokana na kwamba wasanii wengi wa bongo wana tabia na mazoea ya kutafuta kiki mpaka na mambo yenye ukakasi mkubwa mpaka kuitana majina kama mbwa.