Wafahamu vipusa waliowahi kutoka kimapenzi na Harmonize

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuja kutambulika takriban mwongo mmoja uliopita na tangu wakati huo mahusiano yake yamekuwa hadharani.

•Siku za hivi majuzi Harmonize ameonekana akijaribu kumbembeleza mwigizaji huyo amrudie huku akisema anajuta kumkosea.

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Kwa miaka mingi, maisha ya mahusiano ya staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize yamekumbwa na utata si haba.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuja kutambulika takriban mwongo mmoja uliopita na tangu wakati huo mahusiano yake yamekuwa hadharani.

Mahusiano ya kwanza ya Harmonize kujulikana hadharani yalikuwa na mwanamitindo Jacqueline Massawe Wolper.

Wawili hao walichumbiana kati ya mwaka wa 2016 na 2017 kabla yao kutengana katika hali tatanishi.

Wolper alimnyooshea Harmonize kidole cha lawama baada ya mahusiano yao kugonga ukuta huku akimshtumu kwa kukosa uaminifu katika ndoa.

Hata hivyo, takriban miaka miwili iliyopita, Harmonize alijitokeza kupuuzilia mbali madai hayo na kudai kwamba Wolper alikuwa na mazoea ya kutoka nje ya ndoa mara kwa mara.

Harmonize alisema Wolper hakuheshimu mipaka ya mahusiano yao na hata aliwahi kummezea mate aliyekuwa bosi wake katika Wasafi, Diamond Platnumz.

Jacque Wolper
Jacque Wolper
Image: INSTAGRAM

Baada ya kutengana na Wolper, Harmonize alijitosa kwenye mahusiano na mlimbwende kutoka Italia, Sarah Michelotti.

Wawili hao walichumbiana kati ya 2017 na 2020 ambapo waliamua kuenda njia tofauti. Huba lilikuwa limekolea kwenye ndoa yap ya takriban miaka minne ila haikuweza kudumu.

Sarah alimtema msanii huyo baada ya kugundua kwamba alikuwa amecheza karata nje ya ndoa na hata kupata mtoto na mwanadada mwingine.

Mwaka jana, Harmonize alikiri kumcheza Sarah alipokuwa amesafiri kwenda kwao Italia na katika harakati hiyo akampachika mimba mwanadada aliyejihusisha naye.

Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake Sarah Michelotti
Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake Sarah Michelotti
Image: THE STAR

Official Shanteel, kama anavyojitambulisha Instagram ndiye mwanadada ambaye Harmonize alitoka naye kimapenzi na kupata naye mtoto mwaka wa 2019.

Harmonize alimficha mwanawe kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba na hatimaye kumfichua  hadharani Desemba, 2020.

Ufichuzi wa Harmonize ulizua ugomvi kati yake na Sarah na kuchangia kutengana kwao.

Baada ya Harmonize kutemwa na Sarah aliingia kwenye  mahusiano mengine na mwigizaji Fridah Kajala Masaja.

Wawili hao walichumbiana kwa kipindi kifupi mwaka wa 2021. Waliweka mahusiano yao wazi mwezi Februari, 2021 ingawa tayari walikuwa wameanza kuchumbiana awali kabla ya kujitokeza.

Harmonize na Frida Kajala
Harmonize na Frida Kajala
Image: HISANI

Takriban miezi miwili tu baada yao kujitokeza kama wapenzi mahusiano yao yalifika kikomo katika hali tatanishi.

Walipokuwa kwenye mahusiano, Harmonize na Kajala walikuwa wamechora tatoo za majina yao kama ishara ya mapenzi makubwa kati yao. Hata hivyo wote walizifuta tatoo hizo baada ya kutengana.

Siku za hivi majuzi Harmonize ameonekana akijaribu kumbembeleza mwigizaji huyo amrudie huku akisema anajuta kumkosea.

Novemba mwaka jana, Harmonize alitambulisha kipenzi chake kipya kutoka Australia, Briana Jai. Konde Boy alimtangaza Briana kama malkia mpya kwenye ufalme wake huku akiahidi  kumpenda na kumlinda.

Harmonize na Briana
Harmonize na Briana
Image: istagram/briana

Wawili hao hata hivyo walitangaza kutengana kwao hivi majuzi baada ya kuwa pamoja kwa takriban miezi mitano.

Briana alifichua  kuwa vipaumbele vyao katika maisha vilikosa kuwiana na ndiposa wakaafikiana kutengana.