Hajui kuimba, yule ni mzee, Mwijaku amlipua H Baba

Muhtasari

• Kauli ya Mwijaku imejiri baada ya H Baba kusema kwamba Harmonize hakumsapoti katika muziki wake.

• Amemtaka mambo ya kimsingi kuendeleza maisha yake.

Mwanahabari na mfanyibiashara kutoka Tanzania, Mwijaku amemtupia maneno makali msanii H Baba ambaye alisema kwamba Harmonize hakumsapoti katika kazi zake za muziki.

Mwijaku alisema kwamba H Baba hajui kuimba na kuwa anapaswa kujishugulisha a mambo ya kimsingi ili kuendeleza maisha yake na ya familia yake.

H Baba alikuwa akilalamika kwamba Harmonize hakuwahi kumpost yeye ama kazi zake katika mitadao ya kijamii.

Kulingana na Mwijaku, sio jukumu la Harmonize kumpost mtu yeyote na kwamba anapaswa kufanya hivyo kwa hiari yake.

"...Anataka Harmonize ampost kwani yeye ni mwanamke? Wanawake ndo hulia ili wapostiwe, yule aende akafanye mambo ya kimsingi," Mwijaku alisema.

Mwanahabari huyo alisema kwamba H Baba hana lolote la kumlipa Harmonize hata kama atampost a kumsapoti.

Aidha, alishikilia kwamba sio jukumu la Harmonize kuishi vizuri na kila mtu ila anapaswa kuchagua watu ambao waasaidiana kusonga mbele.

"..Nitafutie tajiri mmoja aliyefanikiwa kwa kuishi na watu, hakuna ndugu yangu," Mwijaku aliongezea.

Kwa sasa tutakuwa tunasubiri iwapo H Baba atamjibu Mwijaku kuhusu madai hao.