Mwijaki ahuzunika Alikiba kukosa kwenye tuzo za BASATA

Muhtasari

• Amesema kwamba Alikiba ni msanii mkubwa na alistahiki kujumuisha katika kitengo cha msanii bora wa mwaka.

• Aliwataka BASATA kufanya marekebisho kwenye orodha hiyo. 

Mwijaku
Mwijaku
Image: instgram/mwijaku

Mwanahabari kutoka taifa la Tanzania, Mwijaku ameonyesha kutofurahishwa kwa BASATA baada ya Alikiba kukosekana kwenye orodha ya wasanii bora wa mwaka.

Mwijaku alisema kwamba sio haki Ben Pol kuwepo kwenye orodha ya wasanii bora wa mwaka na Alikiba kukosekana , kwa kile alichokisema kwamba Alikiba alifanya kazi kubwa katika mwaka wa 2021.

Alisema kwamba ngoma ya UTU yake Alikiba ni kubwa mno na ilipaswa kujumuishwa kwenye orodha ya ngoma bora.

"UTU inakosekana vipi kuteuliwa? Labda sio wimbo wa Tanzania ama Bongo fleva?" Mwijaku aliandika.

Kulingana na ujumbe mrefu aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Mwijaku alisema kwamba shirikisho hilo linakosa vipengele vya umakini katika mchakato wa kuandaa tuzo hizo.

Aliendelea pia kuwataja wasanii kama Marioo na Jay Melody ambao walitoa nyimbo nzuri ila zikakosa kuingia kwenye orodha hizo.

Baadhi ya mashabiki walimtaka Alikiba kutojihusisha na tuzo hizo wakisema kwamba atakuwa anajishusha viwango vyake.