(+Video) Akothee awezwa na hisia huku akiwaona watoto wake baada ya miezi 8

Muhtasari

•Akothee aliwapokea Fancy Makadia, Prince Ojwang na Prince Oyoo katika uwanja wa ndege Jumamosi asubuhi .

•Mama huyo wa watoto watano alisema watoto wake ndio zawadi kubwa zaidi amewahi kupokea maishani.

Akothee na familia yake
Akothee na familia yake
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Hatimaye mwanamuziki na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu kama Akothee anaweza kufurahia wakati na familia yake yote baada ya watoto wake watatu wa mwisho kurejea nchini.

Akothee aliwapokea Fancy Makadia, Prince Ojwang na Prince Oyoo katika uwanja wa ndege Jumamosi asubuhi kwa shangwe kubwa. Alikuwa ameandamana na mpenzi wake Nelly Oaks pamoja na mabinti wake wakubwa Vesha Okello na Rue Baby.

Mama huyo alipakia video akiwapokea watoto hao wake na kusema imekuwa miezi minane tangu mara ya mwisho kuonana nao uso kwa uso.

"Imekuwa miezi 8. Ni muda mrefu sana kusubiri wakati huu. Mungu awatie nguvu wazazi wote wanaofanya kazi mbali na familia zao ili kujikimu kimaisha," Akothee alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mama huyo wa watoto watano amesema watoto wake ndio zawadi kubwa zaidi amewahi kupokea maishani.

Fancy Makadia ambaye ni mtoto wa tatu wa Akothee amekuwa akiendeleza masomo yake katika mojawapo ya vyuo vikuu vya kifahari jijini Paris, Ufaransa.

Prince Oyoo na Prince Ojwang pia wamekuwa wakiishi huko Ufaransa na aliyekuwa mpenzi wa Akothee na ambaye pia ni baba ya Oyoo.