(VIDEOS) Ni kuoga na kurudi sokoni! Pritty Vishy apata mpenzi baada ya kuachwa na Stivo Simple Boy

Muhtasari

• Aliyekuwa mpenzi wa Stivo Simple Boy, Pritty Vishy hatimaye amepata mpenzi mpya baada ya kunyang'anywa Simple Boy na Adasa.

Pritty Vishy na mpenzi wake mpya
Pritty Vishy na mpenzi wake mpya
Image: Instagram screengrabs///Pritty vishy

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Stivo Simple Boy, Pritty Vishy hatimaye ametafsiri barabara methali ya Yakimwagika hayazoleki na kukubali matokeo ya kuachwa na mwanamuziki huyo.

Mwanadada huyo baada ya kuweka wazi kwenye Instagram yake kwamba Simple Boy amemuacha na kuendela kidosho wa pwani ya Kenya ambaye pia ni mwanamuziki Adasa, sasa Vishy amerudi sokoni na kuangukia penzi jipya tena, wiki mbili tu baada ya drama za kuachana na mwanamuziki wa Kibera.

Katika msururu wa video ambazo kwa siku mbili sasa amekuwa akizipakia kwenye TikTok yake wakiwa pamoja na mpenzi huyo wake mpya, inaonekana kabisa Pritty Vishy ameirudisha furaha yake baada ya moyo wake kunasa kwa kijana huyo.

Bado haijajulikana kama ni kweli wawili hao waliachana ama ni kiki walikuwa wakitafuta haswa ikizingatiwa kwamba siku moja baada ya madai kwamba Simple Boy ameangukia penzi kwa Adasa, waliachilia kibao pamoja na kuzua uvumi kwamba labda ni kiki tu za mitandaoni na wala si kuachana na Pritty Vishy.