Colonel Mustafa: Nilikuwa nakaa kinyozi saa mbili, maisha yakanilemea, siku hizi dakika 10 tu basi!

Msanii huyo alieleza kupotea kwake kutoka mitandaoni ni kutokana na kuona maisha ya humo ni bandia.

Muhtasari

• “Mitandao ina mambo mengi bandia na ya kutia chumvi, halafu pia kuna shinikizo, ndio maana mimi niliona haina haja niendelee kukaa kule" - Mustafa Colonel.

Msanii mkongwe kutoka Ogopa Djs, Coonel Mustafa
Msanii mkongwe kutoka Ogopa Djs, Coonel Mustafa
Image: Colonel Mustafa (Instagram)

Mwanamuziki Colonel Mustafa ambaye sasa amerudi kwenye gemu baada ya kimya cha muda mrefu, amezungumzia kimya chake na kupotea kwake kutoka mitandaoni muda fulani hapo nyuma.

Alisema kwamba baada ya akaunti yake ya Instagram idukuliwe, alikufa moyo na mambo ya mitandaoni na hivyo kuamua kuchukua likizo kabisa ambayo ilimpoteza kutoka kwa mashabiki wake.

Mustafa amekuwa katika ‘media tour’ kwa takribani wiki moja iliyopita ambapo amekuwa akinadi ujio wa albamu yake ambayo inatarajiwa kutoka mwishoni mwa mwaka huu au mapema mwaka kesho, na katika mahojiano mengi, amekuwa akibanwa na maswali ambayo yamembidi kufunguka kilichomkuta.

Pia alizungumzia kile kilichomchukiza na mitandao ambapo alisema ni vitu vingi vinakuwa vimechagizwa, wasanii kuishi maisha ambayo si yao mitandaoni hali ya kuwa kiuhalisia wanateseka sana.

“Mitandao ina mambo mengi bandia na ya kutia chumvi, halafu pia kuna shinikizo, ndio maana mimi niliona haina haja niendelee kukaa kule, lakini tena kwa sababu ya aina ya hii kazi ya kimuziki, sina jinsi, ndio maana niliona tu nirudi ndio mashabiki wangu waweze kunifikia,” alisema Mustafa.

Alisema kwamba ukiishi maisha ya kudanganya mitandaoni, matarajio kutoka kwa mashabiki yanakuwa mengi mtu anafikiria labda una ndege kumbe maskini wa Mungu hata baiskeli ndio kabisa hujafikia.

Msanii huyo pia alipata kuchekesha pale aliposema kwamba zamani akiwa anaimba sana alikuwac anaenda kinyozi na kukaa hata saa mbili lakini baada ya kukumbana na mambo mengi maishani siku hizi kinyozi hata dakika kumi zinamtosha kumaliziwa.

“Mimi kinyozi kisela sela tu, nafika pale napigwa pigwa, lakini nilibadilika. Zamani nilikuwa nakaa hata saa mbili lakini baada ya kupitia mengi katika maisha, siku hizi hata dakika kumi zinanitosha kabisa nashukuru Mungu kwa uhai,” alisema kwa sauti ya kujiaminia kabisa Colonel Mustafa.

Mustafa alidokeza kwamab uwepo wake kwenye filamu ya uhalisia ya Nairobi Diaries kulimvurugia maisha pakubwa, kulimpotezea dili kibao pamoja na kuivunja ndoa na mke wake wa awali baada ya kusingiziwa kuwa katika mahusiano na Noti Flow, jambo ambalo baadae kwa minong’ono mingi ilibidi tu waanze hayo mahusiano ili kuwazima wambea.