Mwimbaji wa Nigeria Guchi ajibu madai hakuweza kumudu kulipa hoteli Nairobi

Alifichua katika mahojiano kwamba alichagua kuwa na kipindi nchini Kenya kwa sababu anajua kwamba ana mashabiki wengi hapa.

Muhtasari
  • Guchi aliahidi kutumbuiza kwa njia ambayo itamfanya abaki katika kumbukumbu za Wakenya
  • Pia alisema kuwa atafanya miradi kadhaa na wasanii wa Kenya kabla ya kurejea Nigeria
  • Kumekuwa na tetesi kuwa Guchi alikwama jijini Nairobi baada ya kushindwa kulipia chumba cha hoteli
GUCHI
Image: HISANI

Ugochi Lydia Unuoha almaarufu Guchi ni mwimbaji wa Nigeria ambaye alipata umaarufu katika bara zima la Afrika kwa sababu ya wimbo wake maarufu "Jennifer".

Alitua nchini Kenya siku chache zilizopita na alikaribishwa vyema kwenye uwanja wa ndege na vyombo vya habari vya mtandaoni na wasanii wa Kenya.

Alifichua katika mahojiano kwamba alichagua kuwa na kipindi nchini Kenya kwa sababu anajua kwamba ana mashabiki wengi hapa.

Kwamba Wakenya wamemtaka mara kwa mara kuwatembelea  hivyo akaamua kutimiza matakwa yao.

Guchi aliahidi kutumbuiza kwa njia ambayo itamfanya abaki katika kumbukumbu za Wakenya.

Pia alisema kuwa atafanya miradi kadhaa na wasanii wa Kenya kabla ya kurejea Nigeria.

Kumekuwa na tetesi kuwa Guchi alikwama jijini Nairobi baada ya kushindwa kulipia chumba cha hoteli.

Alijibu madai haya kwa kusema kwamba yeye sio 'broke'. Kwamba ana pesa za kutosha kulipia malazi mazuri kwa siku atakazokuwa nchini Kenya.

Guchi alisema kuwa watu hawakuelewa kilichotokea. Kwamba alikuwa amepanga nafasi ndogo ambayo inaweza kuchukua watu wawili tu lakini timu nyingine ilijiunga naye. Ilibidi atafute nafasi kubwa ambayo ingewatosha wote.