Alikiba: Siwezi enda kumuona R Kelly jela hata nikapewa nafasi, vitendo vyake sivisapoti!

Alikiba aliwahi shirikishwa katika kibao na R Kelly miongoni mwa wqasanii wengine wa Afrika.

Muhtasari

• "Vitu alivyovifanya mimi siwezi kuviunga mkono. Mimi binafsi nitaona aibu,” - Alikiba

Wasanii R Kelly na Alikiba
Wasanii R Kelly na Alikiba
Image: Maktaba

Msanii mkongwe katika gemu la bongo fleva, Alikiba ameweka wazi hisia zake kuhusu hukumu ya msanii kutoka Marekani, R Kelly ambaye alifungwa wiki chache zilizopoita kutokana na kesi ya muda mrefu iliyokuwa inamhusisha na unyanyasaji wa kingono.

Akizungumza katika mahojiano ya kituo kimoja cha redio nchini Tanzania, Alikiba alisema kwamba akipata nafasi ya kumtembelea R Kelly gerezani, atakubali kuenda lakini hajui kabisa atamwambia nini nguli huyo wa zamani wa muziki kwa sababu vitendo alivyohukumiwa navyo ni vya aibu na wala yeye haviuingi mkono kabisa.

“Nikipata nafasi ya kumtembelea R Kelly gerezani nitaenda lakini sijui nitaongea naye nini, vitu alivyovifanya mimi siwezi kuviunga mkono. Mimi binafsi nitaona aibu,” alisema mkurugenzi huyo wa Kings Music rekodi lebo.

Vile vile Alikiba alizidi kuelezea kwa kusema kwamba kama kutatokea majibu mawili ya kuchagua kati ya kumtembelea R Kelly gerezani na kutuma salamu tu basi atalichagua la pili na kughairi kuenda kuonana naye uso kwa uso.

“Labda ni vizuri kutuma salamu kuliko kuenda kuonana naye,” Alikiba alisema.

Ikumbukwe Alikiba aliwahi shirikishwa katika kibao kimoja na msanii huyo miongoni mwa mastaa wengine kama vile Navio, Amani, 2face Idibia, Fally Ipupa miongoni mwa majina mengine makubwa kutoka bara la Afrika kwa kibao kali kilichovuma kwa jina ‘Hands Across The World’

Msanii R Kelly alihukumiwa wiki juzi baada ya kupatikana na hatia ya kutumia ustaa wake kuwanyanyasa wanawake na watoto kingono pamoja na kuonesha picha za utupu wao.