Je kusajili Wasanii wa Kike wapya WCB kutaleta ugomvi kati ya Diamond na Zuchu?

Msanii mkongwe DuduBaya alimtaka Diamond Kuongeza wasanii zaidi wa kike kwenye lebo ya Wasafi.

Muhtasari

• Dudu Baya katika mahojiano na wakuza maudhui alimtaka Platnumz kusaini wasanii wa kike ili kuleta usawazishaji wa jinsia kwenye lebo.

• Alidai kuwa kwa sasa msanii  Zuchu ndiye pekee wa kike kwenye lebo hiyo na anahitaji ushindani ili kudumisha viwango vyake vya juu kisanaa.

Diamond na msanii wake Zuchu ambaye anadaiwa kuwa kwenye mahusiano naye
Diamond na msanii wake Zuchu ambaye anadaiwa kuwa kwenye mahusiano naye
Image: KWA HISANI

Staa wa Bongo Godfrey Tumaini almaarufu Dudu Baya akihojiwa na wakuza maudhui alidai kuwa Diamond Platinumz anafaa kuongeza wasanii wengine wa kike ndani ya WCB ili umaarufu ya wasani wa kike nchini Tanzania uongezeke.

Alidai kuwa kwa sasa msanii wa kike anayefanya vizuri ndani ya WCB ni Zuchu peke yake, kitu ambacho kinaweza kumfanya kulegeza kamba katika usanii wake

''Atafute tena msichana ama Wasichana wawili  wengine hii  gemu ya Wasichanai ili wawe wengi'' Dudu Baya alisema.

Wakati wa mahojiano hayo, pia aliweka wazi kuwa Diamond amechangia pakubwa  kuibua vipaji nchini Tanzania.

Aliongeza kwamba kina dada wanaofanya miziki ya Kibongo nchini humo huwa wanalaza damu na kupotea ghafla pindi wanaporekodi nyimbo.

''Mtu kama Nandy na Zuchu  ndo sasa wako juu katika kitengo hicho  cha  akina dada''  Dudu Baya alisema.

Wazo hili la Dudu Baya kumsihi Diamond kuongeza Wasanii wengi wa Kike katika lebo ya WCB, ni kutokana na idadi kubwa ya wasanii wa Kiume ndani ya  WCB kushinda wa Kike.

Baadhi ya wasanii wa Kiume ambao walifanya vizuri chini ya lebo ya Wasafi ni pamoja na Harmonize, Rayvanny, Lavalava na Mbosso.

Kwa sasa chini ya lebo ya Wasafi kuna tu wasanii wa kike wawili Zuchu na Queen Darlene ambaye kwa sasa pia haonekani kwa sababu ya majukumu ya kifamilia.

''Zuchu anafanya vizuri katika usanii wake, na yuko  na kipaji kikubwa anazidi kukua kiumri na pia kimuziki, kwa hivyo akiendelea na utulivu ule atafika mbali maana  yuko mahali salama'' alimaliza Dudu Baya.