Mke wa Kobe Bryant ashinda kesi dhidi ya uvujaji wa picha za kifo chake, afidiwa Ksh 1.9Bn

Vanessa aliwashtaki maafisa wa serikali ya kaunti ya Los Angeles kwa kuvujisha picha za kifo cha mumewe Kobe Bryant.

Muhtasari

• Vanessa alikuwa anaogopa picha hizo zitaonyeshwa hadharani siku moja.

• Hofu hiyo ndiyo ilikuwa msingi wa kesi yake.

Marehemu mchezaji wa vikapu Kobe Bryant
Kobe Bryant Marehemu mchezaji wa vikapu Kobe Bryant
Image: maktaba//bbc

Januari mwaka 2020 ni mwezi ambao utakumbukwa kuwa wa kiza kinene katika wapenzi wa mchezo wa vikapu.

Huu ndio mwezi ambao mchezaji wa vikapu maarufu zaidi duniani Kobe Bryant alifariki katika ajali mbaya ya ndege aina ya helikopta ambapo alikuwa akisafiri na bintiye pamoja na watu wengine sita, wote, hakuna aliyesalimika katika ajali ile.

Ila tukio la kufadhaisha ni picha ambayo baadaye ilisambazwa na ambayo ilisemekana kuchukuliwa na maafisa wa polisi waliokuwa miongoni mwa watu wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio na kuchukua picha hizo za Bryant akiwa amefariki. Picha za kuchukiza ambazo zilizua mjadala mkali mitandaoni kuhusu maadili na heshima kwa marehemu!

Hili lilimsukuma mjane wa Bryant, Vanessa kuelekea mahakamani kutaka haki dhidi ya aliyepiga picha hizo kwa kusema kwamab zilikuwa ni za kutia machungu mno na kuumiza moyo wake haswa yeye kama mjane pamoja na watoto wengine waliobaki kwa kuziona zikisambazwa mitandaoni.

Jana, TMZ waliripoti kwamba Vanessa Bryant ameshinda kesi yake dhidi ya maafisa hao wa Kaunti ya Los Angeles ... baada ya jopo la majaji kumi kuamua kuwa ameteseka na ataendelea kuteseka sana kihisia kutokana na picha za tukio la kifo zilizonaswa kwenye simu za rununu za manaibu wa Sheriff wa Kaunti ya 8 L.A. - - picha anazoogopa zitaonyeshwa hadharani siku moja. Hofu hiyo ndiyo ilikuwa msingi wa kesi yake.

Jopo hilo la majaji lilimfidia Vanessa dola za Kimarekani milioni 16 ambazo ni sawa na bilioni 1.9 pesa za benki kuu ya Kenya.

Wawakilishi hao hawakupiga picha tu bali walizisambaza na marafiki, familia na hata watu wasiowajua kwenye baa. Picha hizo zilisambazwa hata kwenye tafrija na maafisa wa zimamoto.

Mawakili wa Kaunti hiyo waliteta kuwa picha hizo hazijawahi kutokea na zimefutwa kutoka kwa simu za rununu zinazohusika ... kwa hivyo hakukuwa na sababu ya hofu kwamba zinaweza kuvuja.

Mchezaji huyo nguli wa vikapu angekuwepo hai Jumanne wiki hii angefikisha umri wa miaka 44.