Nahisi kuokoka nimtumikie Mungu kuokoa vijana waliopotea - Jack Wolper

Muigizaji Mkongwe huyo alidokeza kwamba upako wa Mungu umemzukia na anahisi kutaka kuokoka.

Muhtasari

• “Kiukweli Nafsi yangu inanituma kumtumikia Mungu wangu yani Nitoe ushuhuda" - Wolper.

Amedokeza kuokoka na kuanza kumtumikia nyimbo
JACKLINE WOLPER Amedokeza kuokoka na kuanza kumtumikia nyimbo
Image: INSTAGRAM

Muigizahi mashuhuru wa muda mrefu Jackline Wolper kwa mara nyingine tena chini ya wiki mbili yupo kwenye vichwa vya habari anasumbua kushoto kulia.

Mjasiriamali huyo ambaye ni mongoni mwa waigizaji walioshabikiwa sana kwenye tasnia ya filamu ya Tanzania ikianza miaka ya 2000 wiki jana alipewa hongera zake baada ya kutangaza kwamba amwejifungua mtoto wake wa pili.

Safari hii Wolper anazungumziwa mitandao ya kijamii baada ya kudokeza kwamba amefikia wakati anahisi kwamba upako wa Mungu umetua kichwani mwake na anahisi kama ameitwa kulihubiri neno la Mwenyezi Mungu.

Kupitia Instagram yake, Wolper alidokeza kwamba siku hizi kila baada ya kusikiliza nyimbo za injili huingiwa na nguvu za ajabu zinazompa msukumo wa kutaka kumtumikia Mungu.

Kwenye video hiyo, Wolper anaonekana akifurahia wimbo ambao unachezwa kwenye mgahawa mmoja huku akijivinjari na kuimba sambamba na wimbo huo na kuifuatisha kwa maneno kwamab anahisi ni muda wa kumtumikia Mungu kwa nyimbo za injili sasa.

Kiukweli Nafsi yangu inanituma kumtumikia Mungu wangu yani Nitoe ushuhuda Na Nimuimbie kwa sauti ya juu hadi wanyama wasikie yani Nina hiyo roho Na sijui imetoka wapi. Mungu Tenda Miujiza yako Nikakutumikie wewe kuokoa vijana waliopotea,” Wolper aliandika.

Wengi wa mashabiki wake walifurahia hatua hiyo na kumpongeza kwamba kama kweli roho wa Mungu amemtuma basi asijaribu kukwepa kama Yonah kutoka biblia na ni sharti atii kile ambacho Mungu amemtuma kufanya.

“Amina Jack...utazidi kuyaona mafanikio yako yakikua kwa Kasi ya ajabu kwa neema za Mungu baba Aliye juu,” shabiki mmoja kwa jina Jenita Twins alimhongera.