Unazidi wamama wote nimewahi kuwaoa hapa duniani - Muigizaji Kigosi amwambia mkewe

Vincent Kigosi ni muigizaji mkongwe ambaye wlikuwa wanaigiza na Steven Kanumba.

Muhtasari

• Kigosi alikuwa anamsherehekea mkewe siku yake ya kuzaliwa ambapo alimtungia ujumbe maalumu.

• Najisikia Fahari sana kutamka maneno ya Kukuwish kwenye kumbukizi ya Kuzaliwa kwako - Kigosi.

Muigizaji Mkongwe vincent kigosi amsherehekea mkewe
Muigizaji Mkongwe vincent kigosi amsherehekea mkewe
Image: instagram

Muigizaji mkongwe wa flimau za Bongo Vincent Kigosi amemsherehekea mpenzi wake kwa ujumbe wa kupendeza siku yake ya kuzaliwa.

Kigosi ambaye ni muongozaji wa filamu enzi wakiigiza na muasisi wa filamu na marehemu Steven Kanumba kupitia ukurasa wake wa Instagram amempongeza mkewe kwa kumtaja kuwa ni mtu aliyemheshimisha kwa kumfanya kulibadili jina lake la utotoni na sasa anaitwa baba mwafulani.

“Dakika, Siku, Miezi na Miaka vinaenda kwa Kasi sana na kujongelea uzee ambao unaongeza Hekima, Upendo na Maarifa kwetu. Naweza kuandika maneno yakawa mengi sana na yasiwe na maana kwetu. Mwanamke anayeweza kulibadilisha jina la UTOTO wako na kukufanya UITWE baba Fulani huyo ni mwanamke wa kumpa heshima nyingi hapa Duniani na Akhera,” Kigosi aliandika.

Alizidi kumiminia sifa kwamba anajihisi Fahari kubwa isiyo na kifani kumtakia heri njema za kuzaliwa na kwamba heshima zake kwake ni mara dufu kutokana na ngazi alizolikweza jina lake.

“Mama Watoto wangu wewe ni mama unayezidi wamama wote ambao nilishawahi KUWAONA hapa Duniani. Najisikia Fahari sana kutamka maneno ya Kukuwish kwenye kumbukizi ya Kuzaliwa kwako MIONGO KADHAA ILIYOPITA. Nakutakia kila la heri katika siku ya kumbukizi za kuzaliwa,” muigizaji huyo alitamka.

Wasanii wenzake walikoshwa na maneno haya na wengine mpaka kuzua utani kwamba kwa vile yeye ni mkongwe katika tasnia ya uigizaji, huenda alikabidhiwa maneno hayo kweney moja ya nakala za kuandaa filamu naye akaamua kuyatema kwa mkewe.

“Unaweza kukuta haya maneno alipewa kwenye Script ya tamthilia fulani. Leo kaamua kuyapest hapa,” msanii Madee alimtania.

Umuoe sasa na kumwita Mke sio ujitie mama Watoto,” Haji Manara alimtania pia.

Filamu ipi ya Kigosi unaifagilia kwa sana?