Nameless apiga picha na Nana Owiti, asema King Kaka aliangukia mali safi

Nameless alikuwa ameenda ChatSpot kuendeleza shinikizo la kutaka barabara moja South C kupewa jina la E-Sir

Muhtasari

• Katika picha hiyo, Nameless na Nana Owiti wanaonekana kupasua tabasamu ghaya huku Nameless akitundika macho yake kwenye utosi wa pua la Owiti.

Nameless akiwa pichani na Nana Owiti
Nameless akiwa pichani na Nana Owiti
Image: instagram

Msanii mkongwe kwenye muziki wa Kizazi kipya cha Kenya, Nameless amewaacha wengi wakizua utani mwingi kwenye Instagram yake baada ya kupakia picha ya pamoja akiwa na mtangazaji wa runinga Nana Owiti.

Katika picha hiyo, Nameless alisema kwamba kijana mdogo kwa maana ya msanii King Kaka aliangukia mali safi.

King Kaka ndiye mume wa Nana Owiti.

“Ndugu mdogo aliangukia Mali safi…😊😁🎯❤️👌🏾@nanaowiti,” Nameless aliandika.

Katika picha hiyo, Nameless na Nana Owiti wanaonekana kupasua tabasamu ghaya huku Nameless akitundika macho yake kwenye utosi wa pua la Owiti.

Msanii King Kaka ambaye alitajwa hapa kama mhusika mkuu aliyeangukia bahati ya kipya kinyemi alisema kwa utani kwamba hakuangukia bali waliangukiana kimpango.

“Hapa ni kama tuliangukiana,” King Kaka aliandika.

Owiti kwenye ukurasa wake alidokeza kwamba Nameless alikuwa ameenda katika kituo cha runinga cha Switch ili kushiriki mazungumzo na Owiti katika kipindi cha ChatSpot.

“Mimi ni mtu mwenye ucheshi sana asikuambie mtu, uliza karibu. Hata hivyo msanii mkongwe Nameless na Lenny wa Change.orke alipitia hapa Switch kwenye Chatspot na tukawa na gumzo pevu,” Nana Owiti aliandika.

Nameless pamoja na wakfu wa Change.or wamekuwa mstari wa mbele kushinikiza barabara moja jijini Nairobi maeneo ya South C kupewa jina la msanii mwanzilishi wa rap ya Kiswahili nchini Kenya, E-Sir kama njia moja ya kutambua mchango wake katika tasnia ya Sanaa humu nchini.