Mama Baha amsherehekea mwanawe kwa kufikisha miezi 6

Mama Baha alipata baraka hiyo ya mtoto baada ya kusubiri hatua kwa miaka mingi.

Muhtasari

• Mwigizaji huyo aliwapa watu matumaini kuwa wanachoombea watakipata kwani miujiza hutendeka na kuwa wasife moyo.

Image: Wanjiku Mburu

Mwigizaji wa Machachari Wanjiku Mburu almaarufu Mama Baha amsherehekea mwanawe aliyefikisha miezi sita leo Jumanne Oktoba tarehe 4.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema mwanawe amefikisha miezi sita na ako tayari kuanza kula.

"Heri ya miezi sita moyo wangu," alisema mama huyo aliye na furaha si haba.

Mama Baha alipata baraka hiyo ya mtoto baada ya  kusubiri hatua ya kuwa na familia kwa miaka mingi.

Mwigizaji huyo alichapisha ujumbe kwa mwanawe mwezi uliopita kwenye ukurasa wake wa Instagram kuashiria malezi kwa mtoto wake yamekuwa mazuri mpaka sasa.

Alipopata uja uzito wa mwanawe, Wanjiku alikiri kuwa alishangaa sana wakati alipofahamu kwamba ni mjamzito kwani ni jambo ambalo hakutarajia na miaka mingi ilikuwa imepita bila yeye kupata uja uzito.

Mwigizaji huyo aliwapa watu matumaini kuwa wanachoombea watakipata kwani miujiza hutendeka na kuwa wasikufe moyo.

Alisema kuwa alikuwa anashuku ujauzito wake na bado hakuamini kuwa ana uja uzito hadi alipoona tumbo lake likiwa kubwa ndipo alipoamini.

Wanjiku alisema amekuwa akisubiria sana kuwa mzazi kwa kuwa katika maisha yake yote ameishi kupenda watoto.

"Ni kitu ambacho niliishi kutaka. Hata hivyo nilikuwa nimesema iwapo nitakosa itakuwa sawa tu. Naamini kuwa Mungu hujibu maombi" Wanjiku alisema.

Mwigizaji huyo alisema hakukata tamaa kwa sababu ya upendo wake kwa watoto na kuwa Mungu hujibu maombi.