Kama sijakukalia kichwani, uzito wa mwili wangu usikusumbue - Kinuthia

Kinuthia alipakia picha kadhaa akionesha mwili wake uliovyostawi na kuwa kirumbi cha mtu

Muhtasari

• Wanamitandao walimsuta vikali wengine wakitumia fursa hiyo kumkejeli kwa njia isiyofurahisha kwa kweli.

Kinuthia awasuta wanaokejeli mwonekano wake
Kinuthia awasuta wanaokejeli mwonekano wake
Image: Instagram

MwanaTikTok Kelvin Kinuthia amewachekesha watumizi wa mitandao ya kijamii baada ya kupakia picha zake akiwa ameongeza uzito kweli kweli.

Katika msururu wa picha hizo ambazo alipakia kwenye Instagram, Kinuthia alishambuliwa na wanamitandao kwamba anafaa kufanya zoezi kwa kile mashabiki wake walisema ameongeza unene ambao umemharibu shepu ya mwili wake.

Mwanablogu huyo aliwasuta vikali wote wanaomtaka kupunguza uzito kwa kufanay mazoezi, aliwaambia kwamba uzito wa mwili wake haufai kuwaingia vichwani kwa sababu hakai vichwani mwao.

Alisema uzito wake unafaa kuwasumbua tu ikiwa anawakalia vichwani na kuwafinyilia chini kwa uzito.

“Isipokuwa nimekaa juu ya uso wako, uzito wangu sio kazi yako. Mwisho wa kauli,” Kinuthia aliandika kwa utani mkubwa.

Baada ya mashabiki wake kufungua picha zaidi katika mrundiko huo, mashabiki hao wengi walionekana kumshambulia kwa cheche huku baadhi wakimtetea kuwa haifai watu kushughulika na mambo yake.

“Tumbo kubwa wewe tunatafuta unga ama tunaagalia hii upuuzi wako,” Ibruzlee alimsuta.

Sasa hizi ni nini hata kama tuliambia tujipende,” mwingine kwa jina Mutheuu alimuuliza.

“Sielewi kwa nini watu wanahisi hitaji la kuaibisha wengine kimwili,” Sarah Kariuki alimtetea dhidi ya masimango.

Watu hawajui mwili ya Kinuthia ndio stock yake...Akifanya vituko zake na hio umama yake anapata riziki. Wewe Kaa tu hapo na chuki Yako ya ufalaKinuthia nora fiu,” Njoro wa Maggy alisema kwa utani.