Janet Mbugua asherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe

Alikumbuka kwamba alikuwa akimkumbatia mtoto Huru si muda mrefu uliopita na sasa anakaribia urefu wake.

Muhtasari
  • Mwanahabari huyo mahiri alisema ni heshima, furaha na baraka kuona mwanawe akikua na akamshukuru Mungu kwa kumfikisha Huru kufikia hapa
Janet Mbugua
Image: Hisani

Mtoto wa kwanza wa mwanahabari Janet Mbugua, Huru Ndichu ametimiza mwaka mmoja zaidi.

Huku akimsherehekea, mtangazaji huyo wa zamani wa runinga ya Citizen kupitia kwenye mitandao ya kijamii alimwandikia  mwanawe ujumbe mzito baada ya kufikisha umri wa miaka 7.

Katika chapisho hilo, Janet alishangaa jinsi wakati unavyosonga haraka kwani mtoto wake anakua haraka.

Alikumbuka kwamba alikuwa akimkumbatia mtoto Huru si muda mrefu uliopita na sasa anakaribia urefu wake.

"Dakika moja unawabeba kama watoto wachanga mikononi mwako, inayofuata, wanakaribia urefu wako! (Urefu kutoka kwa baba, bila shaka!) Heri ya  siku ya kuzaliwa, Huru. Wakati ulienda wapi? Tunakupenda zaidi, "aliandika.

Mwanahabari huyo mahiri alisema ni heshima, furaha na baraka kuona mwanawe akikua na akamshukuru Mungu kwa kumfikisha Huru kufikia hapa.

"Siku zote ningesikia wazazi wakimshukuru Mungu 'kwa kumleta mtoto wao hadi hapa' na ninaipata sasa. Kwa sababu ni heshima na furaha na baraka kuwatazama wakikua," aliongeza.

Janet Mbugua ni mama wa watoto wawili, mtoto Huru akiwa kifungua mimba. Mwanawe mwingine ana umri wa miaka minne.