Mwigizaji mbilikimo kutoka Nigeria asherehekea kufikisha miaka 18, watu washindwa kuamini

Mwigizaji Ebube Obi kwa muonekano wa nje ni kama mtoto wa miaka 7 na wengi walishangaa akisherehekea kufikisha miaka 18.

Muhtasari

• Wengi walibaki kushangaa walipotaarifiwa kwamba Obi amehitimu miaka 18 licha ya kuonekana kama mtoto wa miaka chini ya 10.

Mbilikimo ashangaza watu kufikisha miaka 18
Mbilikimo ashangaza watu kufikisha miaka 18
Image: Instagram//Ebube Obi

Ebube Obi ni mwigizaji anayechipukia kwa kasi ya ajabu kutoka taifa la Nigeria ambaye anawakosha wengi kutokana na uigizaji wake lakini pia kwa umbile lake linalomtoa kama mtoto wa chini ya miaka 10.

Wasichokijua wengi ni kwamba Obi ni mtu mzima ambaye wiki chache alisherehekea kufikisha miaka 18.

Mwigizaji huyo mahiri wa Nollywood na mcheshi alipakia picha za kutikisa mitandao ya kijamii alipokuwa akipasua mbarika kuhusu kuhitimu umri halali wa kujirusha pasi na kuzuiwa kisheria.

Mwigizaji huyo amabye pia anajiongeza kama mcheshi mdogo wa Nollywood alitumia ukurasa wake wa Instagram kusherehekea umri wake mpya na kupakia picha za kuheshimu siku hiyo.

“Asante bwana kwa yote uliyonitendea katika maisha yangu ️Nashukuru sana bwana   ni siku yangu ya kuzaliwa 🎂” Ebube Obi aliandika.

Kwa mwonekano wake wa kwanza ambao ulikuwa wa kutarajia enzi mpya, mwigizaji huyo aliwabariki mashabiki wake na mwonekano wa buluu wa kifalme.

Alitoka na nguo nzuri iliyokuwa imejifunika mwilini mwake na ilikuwa na kofia ya urefu wa sakafu na nyongeza ya shingo yenye shanga za dhahabu, inayolingana na kitobo cha kichwa.

Wakati huo huo, baadhi ya mashabiki wake wamekuwa wakishangaa umri wa nyota huyo mdogo wa sinema, huku wengine wakisema kwamab anadanganya huenda hajafikisha umri wa miaka 18.

Kwa muonekano wake kwa mbali mtu wa kawaida anaweza akamchukulia kama mtoto wa karibia miaka 5 hivi, jambo ambalo liliwashangaza wengi alipoweka wazi kwamba amehitimu miaka 18 tayari.