Macelebs waliopata watoto mabinti mwaka 2022

Kutoka Karen Nyamu, Diana Marua, Anita Nderu, Wahu Kagwi miongoni mwa wengine, waliopata watoto mabinti 2022.

Muhtasari

• Hakuna kitu cha kufurahisha kama mtu kumbeba mwanawe tumboni kwa miezi tisa na hatimaye kumuona akiwa salama salimini.

Baadhi ya wanawake waliozaa watoto wa kike
Baadhi ya wanawake waliozaa watoto wa kike
Image: Instagram

Mwaka wa 2022 umekuwa ni wenye Baraka na furaha tele kwa familia za watu wengi maarufu nchini Kenya.

Huu ndio mwaka ambao watu maarufu katika mitandao ya kijamii humu nchini wamejaaliwa kuwapokea watoto wao na kuoa tabasamu katika nyuso za malaika hao.

Katika Makala haya, tunakuandalia orodha ya watu maarufu ambao walibarikiwa na watoto wa kike mwaka huu wa 2022.

Felicity Shiru

Huyu ni mama mpya kabisa mjini ambaye alijaaliwa kupata mtoto wa kike kwa jina Zoey wikendi iliyopita, Novemba 6.

Shiru na mpenzi wake mwanablogu wa YouTube Thee Pluto walitangaza taarifa hizo kupitia kurasa za mitandao yao ya kijamii.

Diana Marua

Rapa na mwanablogu wa YouTube ambaye pia ni mke wa mwanamuziki wa miaka mingi, Bahati Kioko.

Familia hiyo iitangaza wiki moja iliyopita kumpokea mtoto wao wa kike waliyempa jina Malaika.

Wahu

Huyu ni mwanamuziki wa muda mrefu sana nchini Kenya ambaye pamoja na mumewe Nameless ambaye pia ni mwanamuziki aliyekubuhu katika tasnia ya muziki wa Kenya walitangaza kupokea binti wao wa tatu mwezi uliopita. Binti huyo walimuita jina Shiru.

Ivy Namu

Ni mke wa mwanahabari wa kipindi cha 10 Over 10 kinachopeperushwa kwenye runinga ya Citizen kila Ijumaa usiku, Willis Raburu.

Namu alitangaza kupata mtoto wake wa kike mwezi mmoja uliopita, japo hawakuweka jina lake hadharani ila waliweka wazi kuwa ni mtoto wa kike.

 

Anita Nderu

Aliyekuwa mtangazaji katika kituo kimoja cha redio humu nchini, alitangaza miezi miwili iliyopita kupata mtoto wa kike pamoja na mpenzi wake mwenye asili ya Ulaya.

Wawili hao walimpa binti wao jina la Kaya Gacheri na Nderu alitangaza habari hizi kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Grace Ekirapa

Ekirapa ni mke wa mwigizaji nguli, Pascla Tokodi kutoka Kaskazini mwa Kenya. Yeye pia ni mtangazaji katika kipindi cha injili kwenye runinga moja ya humu nchini.

Mwezi Aprili mwaka huu, wawili hao wliweka wazi kuwa wamepata mtoto wao wa kike waliyempa jina Jasmine Ariah.

Karen Nyamu

Mpenzi wa mwanamuziki wa Mugithi, Samidoh. Mapema mwezi Februari mwaka huu, alitangaza kuchukua likizo fupi kutoka kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti ambapo alienda kujifungua binti yake. Nyamu alisema jina la binti huyo ni Wairimu.