Diamond hakuniacha, mimi ndiye nilimuacha! - Tanasha Donna

Mimi ndiye ninayeondoka labda kwa sababu ninahisi mahitaji fulani hayatimizwa - Donna.

Muhtasari

• Ninapenda mpaka wangu. Ninapenda kuwa na nafasi yangu isipokuwa niolewe - Donna alisema.

Diamond na Tanasha Donna
Diamond na Tanasha Donna
Image: Instagram

Kwa mara ya kwanza mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii Diamond Platnumz na jinsi ulivyosambaratika.

Donna alianza kwa kufutilia mbali dhana na uvumi kwamba amewahi bwagwa katika uhusiano na kuweka bayana kwamba hajawahi achwa bali yeye ndiye huacha wapenzi.

Msanii huyo ambaye awali alikuwa mtangazaji alikuwa anajumuika na mashabiki wake kwenye Instagram Live na gumzo lilianza pale mmoja alitaka kujua ni kipi kilifanya uhusiano wake na Diamond kuvunjika.

Shabiki huyo alimuuliza iwapo sasa hivi anachumbiana naye akadinda kujibu na badala yake kuwauliza mashabiki wake wamueleze dalili zitakazomfanya mtu kujua iwapo bado anachumbiana ama ni urafiki wa kawaida tu.

“Je, ninachumbiana? Nadhani niko.” Tanasha alisema, "Unajuaje kuwa unampenda?"

Tanasha alieleza kwamba kusita kwake kueleza kwamba anachumbiana ni kwa sababu,

“Huwezi kujua kama ni kuchumbiana au kufahamiana na mtu fulani. Kuchumbiana ni nini? Je, ni kwenda kwa chakula cha jioni na kupata kujua mtu unaweza kusema kwamba hiyo ni dating? Au ikiwa una shughuli nyingi tofauti au chakula cha jioni nyingi? Ikiwa huo ni uchumba, basi nadhani nina uchumba.” Donna alijibu.

Mwanadada huyo alionekana kudokeza kwamba hayupo tayari kumuonesha mchumba wake hadharani hivi karibuni, iwapo yupo kwa kile alisema kwamba ana nafasi ya uhuru wake na kumpenda mtu hakufai kuwa kila mara mnaonekana naye.

“Ninapenda mpaka wangu. Ninapenda kuwa na nafasi yangu isipokuwa niolewe. Na hata hivyo, napenda bado kuwa na maisha yangu mwenyewe kwa sababu kuwa katika upendo, na wakati unampenda mtu, haimaanishi kuwa anakuwa ulimwengu wako wote. Wewe ni sehemu ya ulimwengu wangu, sio ulimwengu wangu wote, kwa sababu nina marafiki ninaowapenda. Nina familia yangu. Nina uhusiano wangu na Mwenyezi Mungu, na nina mtoto wangu. Nina upande mwingine kabisa wa mimi, kwa hivyo unakuwa sehemu ya ulimwengu wangu. Huwezi kuwa ulimwengu wangu wote, na hapo ndipo mambo yanakuwa sumu,” alifafanua.

Kisha akafichua kwamba yeye huweka mipaka katika mahusiano yanapokuwa na sumu.

"Kusema kweli, sijaribu kujisifu lakini sijawahi kuachwa maishani mwangu. Kamwe. Ni ukweli tu kwamba sijawahi kuachwa."

Aliongeza, "Mimi ndiye ninayeondoka labda kwa sababu ninahisi mahitaji fulani hayatimiziwi au ninahisi kama hatuendani kwenye ukurasa mmoja au kitu kama hicho."