Akothee atetea maamuzi ya maisha yake: Usijaribu kuficha zamani yako

Kila ukurasa katika siku zako za nyuma ulionyesha kitu katika siku zijazo - Akothee.

Muhtasari

• Usijaribu kamwe kuficha au kufuta maisha yako ya nyuma, yakumbatie, hivyo ndivyo Historia iliundwa - Akothee.

Akothee atetea kale yake
Akothee atetea kale yake
Image: Instagram//Akothee

Aliyejitangaza kuwa rais wa akina mama wasio na waume Akothee mzaliwa kama Esther Akoth amewashauri mashabiki wake kuendelea kusukuma mbele malengo yao na kamwe wasifute uzoefu wao wa zamani.

Akichapisha picha yake akitumbuiza miaka kadhaa iliyopita, mama huyo wa watoto watano alisema kwamba watu wanapaswa kutumia uzoefu wao wa zamani kama hatua ya kufikia mambo makubwa zaidi maishani.

Alisema yeye hata sekunde moja hajutii yale yote aliyoyafanya mwanzoni kwani ilikuwa kama njia moja ya kumpitisha hadi kwenye mafanikio yake ya hivi sasa.

“Kila safari lazima ianze na hatua moja, kile unachofikiria ulimwengu unashikilia kutoka kwako, unakishikilia kutoka kwa ulimwengu. Nenda huko nje na utumie nguvu zako 💪 Sijawahi kukutana na mtu yeyote aliyefanikiwa na maisha mepesi ya zamani, yako ya zamani yasifanye kazi au kutumiwa dhidi yako, iwe karatasi zako za marekebisho, kwa sababu zamani tunayo sasa na tunatazamia siku zijazo.” Alisema.

Aliwashauri wafuasi wake kutokwamishwa na mambo ya nyuma wala kutokubali kuhukumiwa kwa kile walichokifanya awali.

Alisema kuwa mtu unapokuwa huru na kukubali makossa yako ya awali ndio mwanzo wa kujifunza kupiga hatua zingine mbele.

“Kila ukurasa katika siku zako za nyuma ulionyesha kitu katika siku zijazo. Usijaribu kamwe kuficha au kufuta maisha yako ya nyuma, yakumbatie, hivyo ndivyo Historia iliundwa. Wale wanaojificha kutoka kwa maisha yao ya nyuma hawana chochote cha kuonyesha katika maisha yao ya sasa, kwa sababu bado wanaishi zamani na kuzikwa katika siku zile zile, wanaweza kusahau wakati ujao kwa kuwa HAWANA. HISTORIA IMETUNGWA NA ZAMANI IKUBALIE,” Akothee alitoa ushauri.

Akothee aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 ili kuolewa na mwanamume ambaye alifikiri ndiye kipenzi cha maisha yake. Kwa maneno yake mwenyewe, alitoka katika familia thabiti lakini aliasi dhidi ya matarajio yaliyowekwa juu yake.

 

Alikaa nyumbani, akifanya kazi kama house girl kwa mama mkwe wake katika kipindi cha miaka saba. Wakati wote huu, mumewe alikuwa shuleni akipata digrii yake.