Unamuitaje Zuchu mke wako wakati hujamuoa? - Mwijaku amuuliza Diamond

"Kwa kuongea uongo kwenye sunnah alio itekeleza mtume wetu muhammad swalla llahu alayh wasalaam,” Mwijaku alisema.

Muhtasari

• Kwa sheria ya kiislaamu tayari UMERITAD inabidi USILIMU TENA UWE MUISLAMU - Mwijaku alimshauri Diamond.

Mwijaku amkaripia Diamond kwa kumuita Zuhcu mkewe
Mwijaku amkaripia Diamond kwa kumuita Zuhcu mkewe
Image: Instagram

Mtangazaji mbwatukaji Mwijaku amemzukia Diamond kwa Makonde na makofi kwa kile alidai kuwa ni msanii huyo kuwavunjia heshima watu walioko kwenye ndoa kwa kumuita Zuchu mkewe.

Kupitia Instagram yake, Mwijaku amemkaripia na kumkoromea vikali Diamond huku akimtaja kama aibu si tu kwa jamii nzima bali pia kwa dini tukufu ya Kiislamu.

Amemtaka Diamond kutubu mara moja kwa sababu haiwezekani kumuita mtu mke wake wakati bado kila mtu anajua ndoa haijafungua – ni kinyume na dini ya Waislamu.

Umetukosea sana sisi tuliopo kwenye ndoa . Nikwambie tu NDOA SIO KWAPA. Unamuitaje zuchu MKE WAKO ? Wakati hauja OA . Kwa sheria ya kiislaamu tayari UMERITAD inabidi USILIMU TENA UWE MUISLAMU. Kwa kuongea uongo kwenye sunnah alio itekeleza mtume wetu muhammad swalla llahu alayh wasalaam,” Mwijaku alisema.

Ishu nzima ilizuka siku ya kusherehekea Zuchu kuzaliwa kwake ambapo mamake Diamond Bi Sandra au kwa umaarufu wake kama Mama Dangote alipoweka wazi kuwa Zuchu ni mkaza mwana wake na hata kumtakia kila la kheri katika siku hiyo hata kama manii huyo bado anaendelea kutusua katika ziara yake ya kimuziki huko Marekani.

Baadae Alhamisi asubuhi Diamond alimwaga mtama kwenye kuku wengi alipopakia picha kadhaa za Zuchu pamoja na video wakiwa pamoja katika madhari ya kutamanisha na kuachia ujumbe mrefu huku akimalizia kumpa hakikisho kuwa siku zote atabaki kumpenda yeye tu.

Mwenyez Mungu akupe baraka na akulinde katika Maisha na safari yako hii ya kuchangia kuonesha Dunia kua WaAfrika tumebarikiwa kipaji kiasi gani… Kumbuka Simba siku zote anakupenda,” Diamond alimaliza kwa hakikisho kuntu.

Katika video nyingine pia iliyosambazwa mitandaoni, msanii huyo anasikika akimwambia Jux kuwa Zuchu ni mke wake pika pakua, tamko ambalo limezua mjadala mkali miongoni mwa mashabiki wake lakini pia kwa waumini wa Kiislamu wanaosema kuwa kumuita mtu kama mkeo wakati hujamuoa rasmi ni kama kufuru.

Maoni yako ni yepi?