Mama Dangote athibitisha Zuchu ni mpenzi wa Diamond, amtakia heri ya kuzaliwa

"Mamamkwe Zuhura Othman Suod @officialzuchu 💕💕💕," Mamake Diamond aliandika.

Muhtasari

• Mama Dangote alimtakia mwanamuziki huyo mema maishani mwake anapoanza ukurasa mpya wa maisha yake.

•  Msanii huyo wa WCB Wasafi alipakia picha zake akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na marafiki zake.

Image: INSTAGRAM// ZUCHU, MAMA DANGOTE

Mamake mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz, Mama Dangote amedhibitisha kuwa Zuchu ni mke wa mtoto wake Diamond Platnumz.

Kwenye Instagram, Mama Dangote alipakia video ya Zuchu huku akimsherehekea na kumtakia heri ya kuzaliwa.

Alisema jinsi anavyomtakia mwanamuziki huyo mema maishani mwake anapoanza ukurasa mpya wa maisha yake.

"Nakutakia maisha marefu yenye Baraka... Ma mkwe Zuhura Othman Suod @officialzuchu 💕💕💕," Mamake Diamond aliandika.

Zuchu alimjibu Mama Dangote na kumshukuru kwa kumtakia mema.

"❤️❤️❤️ asante mamaangu 😍😍," Zuchu alisema.

Msanii huyo wa Diamond alipakia picha zake akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na marafiki zake.

Alisema kuwa marafiki zake walimpangia siku hiyo na kuhakikisha kuwa amesherehekea vilivyo siku hiyo.

"Bday Dump Asante kwa marafiki zangu maana sikutaka sehemu yoyote ya hii😂😂 ila walinivuruta ili nisherehekee🫶 Nawapenda nyote, nilifurahia siku hiyo na ilikuwa ya kipekee, asante 🙏 @dorice_mziray @angelnyigu @karenito__ @djkidylax," Zuchu aliandika.

Hivi majuzi, kwenye akaunti yake ya snapchat, Zuchu alionyesha viatu vya bluu ambavyo alinunuliwa na mama huyo anayedaiwa kuwa mama mkwe wake.

Katika maelezo ya video, binti huyo wa Khadija Kopa alieleza shukrani zake za dhati kwa Mama Dangote na kudokeza upendo wake kwake.

"Mamangu Mama Dangote Asante🥰😍," aliandika.

Kitendo cha Mama Dangote ni kiashirio tu cha upendo mkubwa na muunganiko mzuri kati yake na msanii huyo wa Wasafi.

Jana, Jumanne, Zuchu pia alidhibitisha mahusiano yake na Diamond na kufichua kuwa ni mpenzi wake.