Olunga apigwa na butwaa kununua mboga Ksh 600 kwa fungu moja Qatar

Mama mboga anavuna sana. Furaha kwa wakulima wetu wa Kenya - Olunga.

Olunga anunua mboga shilingi 600 kwa fungu moja
Olunga anunua mboga shilingi 600 kwa fungu moja
Image: Facebook

Mchezaji wa kimataifa wa Kenya anayesakaja soka ya kulipwa nchini Qatar, Michael Olunga alipigwa na butwaa baada ya kuingia kwenye duka moja la jumla la kuuza vyakula na kupata mboga aina ya Sukuma Wiki zinauzwa kwa shilingi 600 pesa za Kenya kwa mtungo mmoja.

Mshambulizi huyo hatari anayechezea Al-Duhail SC ya Qatar alichapisha picha yake akiwa katika duka kubwa la Qatari Carrefour kwenye ukurasa wake wa Facebook mnamo Jumanne, Desemba 6.

Picha hiyo ilimwonyesha akiwa ameshikilia rundo la Sukuma wiki ya kijani na safi, ambayo alikuwa ametoka kuichukua kwenye rafu.

Akinukuu, Olunga alifichua kwamba fungo dogo la Sukuma wiki ya Kenya, ambayo haiwezi kulisha zaidi ya watu watatu, ilikuwa ikiuzwa kwa KSh 600. Alionyesha mshangao mkubwa kwamba

"Kale ya Kenya (sukuma wiki) 18.25 kwa fungo (takriban Ksh 600). Wueeeh!!!Ni ukweli Inakata pande zote mbili," Oling aliandika.

Alienda kwenye sehemu ya maoni ya chapisho hilo na kusema kuwa anafuraha kwa wakulima wa Kenya kwa kuwa mauzo yao ya nje yalikuwa yakifanya vyema katika soko la kimataifa. "Mama mboga anavuna sana. Furaha kwa wakulima wetu wa Kenya. Sukuma Wiki ya Kenya inahitajika sana . Imeisha. Hii hapa nilinunua pakiti 5 kwa 91 ( KSh 2700)."

Olunga anaendelea kufurahia mechi za kombe la dunia zinazoendelea nchini Qatar huku akisubiri kukamilika kwa mechi hizo kukamilika kabla ya ligi ya Qatar kurejelewa.

Mchezaji huyo nguli ambaye kwa sasa ndiye nahodha wa timu ya taifa Harambee Stars amekuwa aking’aa kweli kweli kwenye ligi hiyo huku akiibuka mfungaji bora wa katika misimu iliyopita.