Saa hii hata mmoja sina - Pritty Vishy ahuzunika kuwa singo

Vishy alikumba jinsi alivyokuwa kwenye uhusiano mzuri mwaka huu ulipoanza

Muhtasari

• Kwenye Instastory zake Vishy alikuwa na huzuni kwa kuwa hana mpenzi mwaka unapoelekea kuisha.

• Vishy alisema jinsi anavyotaka kuwa huru na aliwaomba msamaha wale ambao amewakosea mwaka huu .

Pritty Vishy
Image: Pritty Vishy Instagram

Pritty Vishy ni anaonekana kuhangaishwa na upweke na sasa ameanza kuwa na kumbukumbu za maisha yake ya hapo awali.

Kwenye Instastory zake Vishy alikuwa na huzuni kwa kuwa hana mpenzi haswa mwaka unapoelekea kuisha.

"Kwani mmeniamuliaje? Nilianza mwaka nikiwa kwenye uhusiano mzuri ila kwa sasa sina hata kamoja," Vishy aliandika huku akiongeza emoji inayolia na jicho moja.

Vishy alionyesha kutamani kuwa kwenye uhusiano na kupendwa na mtu ila kwa sasa hana hata wa kumkumbatia.

Kwenye Instastory zake bado, Vishy alisema jinsi anavyotaka kuwa huru na aliwaomba msamaha wale ambao amewakosea mwaka huu .

"Kwa kuwa mwezi unaokuja ni mwaka mpya, nataka kuchukua fursa hii kuomba msamaha kwa wale niliokosea kwani nataka kuwa na moyo mwepesi," Vishy alisema.

Wanamitandao wamekuwa wakihisi kuwa huenda Vishy aliachwa na  mpenzi wake baada ya kupakia ujumbe akieleza jinsi amevuja moyoni.

Hivi majuzi, aliwakanya wanawake dhidi ya kujibadilisha kwa ajili  ya kutaka kupendwa na wanaume kwani hata wakijibadilisha bado wanaume hawatatosheka.

Vishy alikuwa akichumbiana na mwanamuziki Simple Boy kabla ya kuwa mastaa maarufu, walikuwa wamekuwa katika uhusiano tangu wakiwa darasa la 8.

Simple Boy alikuwa amefichua kuwa alikuwa anamgoja Vishy amalize shule kisha waoane.

Hata hivyo, baada ya kuwa mastaa, wapenzi hao walitengana huku Vishy akidai kuwa mwanamuziki huyo hakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yake binafsi na alifanyiwa na wakubwa wake.

"Labda kuna mtu anayenifaa huko nje na naendelea kujisukuma pale. Labda yeye ako na mtu mwenye  atakuja kumfungua akili haraka kuliko  vile nilivyojaribu na najaribu kuzuia. Wacha aende huko nje ajaribu nami nijaribu" alisema.

Baadaye, Vishy alitangaza kuwa kwenye uhusiano na mwanamuziki Madini Classic ila ilifichuka kuwa kiki ya wimbo alioachia, Vishy akiwa vixen wake.