Hisia mseto baada ya Pritty Vishy kusema wanaume hawatosheki

Vishy aliwasihi wanawake wasijibadilishe kwa ajili ya mwanaume

Muhtasari

β€’ Vishy alisema kuwa hata mwanamke ajaribu kiasi gani kujibadilisha ili ampendeze mwanaume bado ataenda nje ya ndoa.

β€’ Wengi walikubaliana naye na kusema kuwa wazo hilo alilotoa ni la busara sana huku wengine wakipingana naye .

Pritty Vishy
Image: Pritty Vishy Instagram

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Simple Boy, Pritty Vishy amezua gumzo mtandaoni baada ya kuandika ujumbe akisema kuwa wanaume wakiwa kwenye uhusiano hawatosheki.

Kwenye Instagram, Vishy aliweka picha yake na kuandika ujumbe huo ambapo alikuwa anawashauri wanawake.

Aliandika ujumbe huo ili kuwakumbusha wanawake kujipenda walivyo na kukataa kujibadilisha kwa ajili ya wanaume.

"Wanaume huwa hawatosheki. Usimruhusu mwanaume yeyote kubadilisha sifa zako, umbo au hata kazi yako ili aweze kuwa nawe," Vishy alisema.

Vishy alisema kuwa hata mwanamke ajaribu kiasi gani kujibadilisha ili ampendeze mwanaume bado ataenda nje ya ndoa.

"Mwanaume atakuwa na mke mzuri, mwenye umbo zuri, wa kifahari nyumbani na bado ataenda nje ya ndoa au kuwa na uhusiano na mwanamke mnene, asiye na umbo la kuvutia na ni mfanyikazi wa nyumbani. Ujumbe mkuu hapa ni usimruhusu mwanaume yeyote akuambie cha kufanya na umbo unalofaa kuwa nalo ili kuwa naye juu bado ataenda nje," alisema.

Wengi walikubaliana naye na kusema kuwa wazo hilo alilotoa ni la busara sana huku wengine wakipingana naye .

"Matako nayo nitaongeza pthoooooπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œ," karls_achyeng alisema.

"Kulingana nami, chochote atakachosema nitafuataπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚," owande_I_santana aliandika.

"Wanawake msidanganywe, mambo huaribika ikiwa una urembo bila akili," harl_marcx aliandika.

Wengine hata hivyo walimkejeli na kusema kuwa anawazungumzia vibaya wanaume kwa kuwa ameshindwa kuwa kwenye uhusiano na mwanaume.

"Nilijua tu utachezwa....πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚..malipo ni hapa chini ya jua ulimcheza stivo ukaona wee ni MamayaoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚,"palmer_photography 254 alisema.

"πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈ kwani amekuacha yawa," beryl.brown alisema.

Vishy alichumbiana na Simple Boy kutoka walipokuwa darasa la 8 ila baada ya mpenzi huyo wake wa hapo awali kuvuma na kuwa mtu maarufu walitengana.