Sitaki mke tena! Daddy Owen asema baada ya kukosa 'kienyeji'

Daddy Owen alisema kuwa ametosheka na maisha yake bila mke

Muhtasari

• Mwimbaji huyo alisema pia kuwa hamtaki mke wa kumwandalia chakula kwani anaweza kula chakula hotelini.

• Zaidi ya hayo, alifichua pia kuwa hajajihusisha na kitendo cha kufanya mapenzi kwa miaka miwili, jambo ambalo linamhakikishia kuwa yuko sawa bila mwanamke maishani mwake.

Daddy Owen
Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Daddy Owen, amesema kuwa ameacha kutafuta mke wa kutulia naye hata baada ya harakati zake za bidii za kutafuta mke.

Kwenye mahojiano yake na mwanahabari, Daddy Owen alisema kuwa kwa sasa ametosheka na maisha yake ya kuwa singo.

"Kwa sasa nafanya mambo mengi, sitafuti tena mke. Nitafute mke wa nini? Kama ni mtoto ninaye tayari, si bora kuwa na mtoto," Owen alisema.

Alieleza kuwa amesitisha jambo la wanawake kumtumia ujumbe wa kutaka kuwa mke wake kwa kuwa yuko sawa bila.

Mwimbaji huyo alisema pia kuwa hamtaki mke wa kumfanyia kazi za nyumba au kumwandalia chakula kwani anaweza kula chakula hotelini.

"Mwanaume akifika miaka fulani anahisi kuwa ametosheka na yale ako nayo, nina mtoto na nimetosheka na hayo . Nilishaoa kitambo na haikufaulu, niko sawa hivi," baba huyo wa watoto wawili alisema.

Zaidi ya hayo, alifichua pia kuwa hajajihusisha na kitendo cha kufanya mapenzi kwa miaka miwili, jambo ambalo linamhakikishia kuwa yuko sawa bila mwanamke maishani mwake.

"Kampeni ya kutafuta mke wa kuoa imeisha," alisema.

Hivi majuzi, mwimbaji huyo alikuwa ametangaza kuwa anatafuta mke wa kuoa na kusisitiza kuwa anataka tu msichana wa kijijini.

Owen alisema pia hataki mwanamke ambaye yuko mtandaoni wala anayetoka mjini kwani ni wajuaji sana.

Alikuwa anataka mwanamke huyo awe mweusi tititi na mcha Mungu.

Mabinti wengi akiwemo aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Simple Boy, Pritty Vishy, walimtumia Owen ujumbe wakitaka kuwa mke wake.

Owen hata hivyo ameonekana kuchoshwa na kutafuta mke na kuamua kutulia na kuendelea na maisha yake.