Sababu ya Harmonize kuachwa na Kajala hii hapa, mtama umemwagwa kwa kuku wengi!

Mtangazaji wa Wasafi Diva thee Bawse alimwaga ubuyu wote kuanzia A mpaka Z kuhusu sakata zima.

Muhtasari

• Juzi Kajala alidhibitisha kuachana na Harmonize ila hakutajqa sababu za kuvunja mahusiano yao.

• Ikumbukwe wawili hao mwezi Juni walivishana pete za uchumba na mashemeji wa mitandaoni walikuwa wanasubiria ndoa.

Harmonize na Kajala
Harmonize na Kajala
Image: Instagram

Sakata la Harmonize kuachwa na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu Kajala Masanja limezidi kutokota na kuchukua mkondo mwingine.

Za ndani kutoka kwa mtangazaji Diva The Bawse kutoka kituo cha Wasafi zinadai kuwa msanii huyo aliachwa baada ya kumpachika mlupo mimba.

Katika simulizi ndefu kidogo ambayo mtangazaji huyo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, anadai kuwa Harmonize alianza kuenda na maji baada ya kufumaniwa akifanya mazungumzo ya simu na mlupo huyo wake.

Hizi ni habari za kichinichini zinawajia moja kwa moja kutoka kwa Diva kwanza ni Muhtasari wake. ameachwa , ame blockiwa kila Mahali. Mapenzi haya kweli hayana Mwalimu . Mapenzi yanauma,” sehemu ya simulizi hiyo ilisoma.

Bawse aliendelea kusema kuwa Harmonize kitumbua chake kilibuma kwenye mchanga alipofumaniwa na baadae akaanza kuvunja pafyum kutokana na hasira ya kutotaka kuulizwa.

“Alipofumwa anaongea na simu akaulizwa unaongea na nani akalowa ghafla , sehemu Ya Pili alipobambwa ananyata kwa dada , Sehemu Kubwa kuliko ni alipoanza vunja Pafyum za watu ati hasiraaaaa kumbe wee wee 😱... Haya Mambo bwana ... Sijaelewa Kwa nini kaka kavunja sana Pafyum za watu alipofukuzwa ... kaulizwa unavunja umenunua wewe akamind halafu Pafyum brands tu ... Maana unaambiwa Pafyum ziko very expensive zimetoka dubai ... basi jamaa kavunja kwa hasira aaaah no sio hasira .. ni wee wee 😇 Sema Maskini Kijusi kimechomolewa kitumbo cha Miezi 5 ... sema safari hii VUJU VENGA,” Diva alisimulia. 

Juzi Kajala alidhibitisha kupitia ukurasa wake kuwa ni kweli uhusiano wake na Harmonize umefika mwisho, ila hakuendelea kutoa za ndani kiini cha kuvunja uhusiano wake wakati mashemeji wa mitandaoni tulikuwa tunasubiri ndoa baada ya ile shughuli ya kuvishana pete za uchumba.

“Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia,ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia😌. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu. Hakika nimekosea familia yangu, ndugu zangu, na marafiki zangu. Kutenda kosa si kosa, kosa kurudia kosa. Ninamsamehe EX wangu na niko tayari kwa yajayo,” Kajala aliandika.

Kama vipi itabidi umechukua juisi yako ya mkwaju na popcorn kibao, kaa mkao wa kula maana hili picha ndio mwanzo linaanza!