Kajala Masanja ajibu kuhusu kumuacha Harmonize

Kajala alishindwa kujizuia na akamjibu, "unasubiri nini?

Muhtasari

•Mara nyingi, Kajala amekuwa akichapisha picha zake akiwa pekee yake na zingine akiwa pamoja na binti yake wa miaka 20, Paula Kajala.

•Picha ya mwisho ya Konde Boy na Kajala kwenye ukurasa wake wa Instagram ilichapishwa mnamo Oktoba 7.

Harmonize na mchumba wake Kajala Masanja
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Hali ya ndoa ya Harmonize na Kajala bado haijafahamika wazi huku tetesi zikiendelea kuenea kuwa wawili hao hawapo pamoja tena.

Matendo ya hivi majuzi ya wachumba hao haswa kwenye mitandao ya kijamii yamezua wasiwasi miongoni mwa mashabiki wao ambao wamekuwa wakihoji kuhusu kinachoendelea ndani ya mahusiano yao. Japo hawajajitokeza kufafanua iwapo bado wako pamoja au la, posti zao za hivi majuzi zimeendelea kuzua wasiwasi na kuibua maswali zaidi

Mara nyingi, Kajala amekuwa akichapisha picha zake akiwa pekee yake na zingine akiwa pamoja na binti yake wa miaka 20, Paula Kajala.

"Kuwa mpole, kila moyo huficha majeraha mengi ambayo hayatoi damu," muigizaji huyo alisema katika chapisho lake la hivi punde kwenye Instagram.

Kama kawaida, mashabiki walimimika chini ya chapisho hilo na maswali kemkem wakitaka aweke wazi kinachoendelea kati yake na Konde Boy.

"Dada, kama mshaachana nambie niku-unfollow," mtumizi mmoja wa Instagram aliandika chini ya chapisho hilo.

Kajala alishindwa kujizuia na akamjibu, "unasubiri nini?

Maoni mengine mengi chini ya chapisho hilo la Alhamisi ambayo hakujibu yalikuwa kuhusu hali ya ndoa yake.

@mangekimambi.official Konde yuko wapi?

@mis.musyoka Pete iko wapi?

@zananajuice Nasemaje usirudi, jua ni kali sanaaa khaa

@deosambala Mtuambie kama mmeachana ni kuunfollow, sitaki maumivu anayopata kakangu niyaone nitakuchamba bure asubuhi jioni

dor_v.i.p Dada Frida eti ni kweli mmeachana na Harmonize au ni figisu

Siku za hivi majuzi, Kajala na Harmonize hawajaonekana pamoja kama ilivyokuwa hapo awali ambapo walichapisha picha zao pamoja kwenye kurasa zao na hata kusifiana na kuhakikishiana kuhusu mapenzi yao kwa kila mmoja.

Picha ya mwisho ambayo Kajala alichapisha akiwa pamoja na Harmonize ilikuwa Novemba 14 ambapo alikuwa akiwashukuru mashabiki wa mwimbaji huyo nchini Uganda kwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha ambazo walifanya.

"Shukran Uganda. Kenya kuweni tayari," aliandika.

Baada ya hapo hajachapisha picha yoyote wakiwa pamoja na hata hajaonekana akimzungumzia mpenzi huyo wake.

Aidha, imebainika kuwa amebalisha bio yake ya Instagram kutoka 'mke wa @harmonize_tz' na kusalia kuwa Mama ya @therealpaulahkajala na mke na meneja.

Harmonize pia ameweza kufuata mkondo huo na kuchukua hatua ya kufuta jina Kajala Masanja kutoka kwa bio yake ya Instagram.

"Baba na mume," bio ya sasa ya staa huyo wa Bongo inasoma. 

Picha ya mwisho ya Konde Boy na Kajala kwenye ukurasa wake wa Instagram ilichapishwa mnamo Oktoba 7.

"Hakuna siku ya kupumzika @kajalafrida❤," maelezo ya picha hiyo yalisoma.

Kajala ambaye pia ndiye meneja mkuu wa Harmonize hajakuwa akitangaza wimbo wa mwisho wa mwanamuziki huyo 'Weed Language' ambao alimshirikisha staa wa dancehall kutoka Jamaica, Konshens.