Uhusiano wa Harmonize na Kajala upo mahututi, adaiwa kumpa Anjella mimba na kumfukuza

Je, uvumi huu kama ni kweli, huenda ndo chanzo cha kudorora kwa mahaba kati ya Harmonize na Kajala?

Muhtasari

• Masha Love alimtemea nyongo Harmonize bila kumtaja jina na kusema kuwa amemkosea sana Anjella kwa kumpa mimba na kumfukuza.

Harmonize adaiwa kumpa Anjella mimba, vipi kuhusu uhusiano wake na Kajala?
Harmonize adaiwa kumpa Anjella mimba, vipi kuhusu uhusiano wake na Kajala?
Image: Instagram

Anjella ana wiki kadhaa tangu aiage familia ya lebo ya Konde Music Worldwide. Lakini licha ya Harmonize kutaja kuondoka kwake kuwa kwa wema, tayari baadhi ya watu wameanza kulitifua timbwiri kali.

Anjella sasa anasemekana kuwa ni mjamzito na kuwa kuondoka kwake Konde Gang kulikuwa kwa shari mno. Uvumi wa ujauzito wake tayari umepewa mhusika mkuu ambaye ni aliyekuwa bosi wake Harmonize.

Balozi wa mauzo Masha Love amekuwa mtu wa hivi punde kutamka uwezekano wa Anjella kuwa mjamzito na hata kutamka waziwazi kuwa aliyempa mimba hiyo ndiye alimpora kila kitu na hata kumfukuza – moja kwa moja kwa wale wanaofuatilia matukio yote wanajua hapa analengwa Harmonize hata bila kutajwa kwa jina.

Masha Love alikuwa anajibu swali na mwanablogu mmoja aliyetaka kujua ushari wake wa Anjella iwapo ana mimba kama yeye – Masha ana mimba ya mwanaume ambaye walichumbiana kwa miezi 8 kabla ya kugundua lijali huyo alikuwa anatoka kimapenzi na rafiki yake na hivyo ndivyo waliachana.

Alitoa ushauri kwa Anjella kuwa aijaribu kuavya mimba hiyo hata kama haihudumiwi kwani hata yeye ana mimba ambayo haihudumiwi na anailea.

“Mfano Anjella ana mimba, mimi namshauri asitoe, mbona hata mimi mimba yangu haihudumiwi! Ila tu huyo aliyempa mimba ndiye aliyemkosea Anjella, sababu hawezi akampa mimba, akampora kila kitu na kumfukuza,” Masha Love alitema moto.

Aliendelea kumlenga Harmonize vikali kwa kusema kwamba hata kama yeye anaangalia uhusiano wake mpya na Kajala, anafaa akumbuke kuwa huyo bado hajamzalia.

“Hata huyo mwanamke ambaye yeye anamlinda huyo, mwisho wa siku yeye ana mtoto, lolote linaweza kutokea hata kwa mtoto wake. Malipo ni hapa hapa duniani,” Alimshambulia pia Kajala.

Sakata la Harmonize kumpa mimba Anjella ni uvumi tu ambao haujadhibitishwa ila kama ni kweli basi hili litakuwa linaibua baadhi ya majibu ambayo wengi wamekuwa wakiuliza kuhusu mwelekeo wa Harmonize na Kajala ambao kwa zaidi ya mwezi sasa hawajaonana wakipetiana na kudekezana kwa mahaba kama awali.