Namsamehe aliyekuwa mpenzi wangu na niko tayari kwa mwingine - Kajala Masanja

Kajala amedhibitisha kutengana na mpenzi wake Harmonize

Muhtasari

• "Hakika nimekosea familia yangu, ndugu zangu, na marafiki zangu. Kutenda kosa si kosa, kosa kurudia kosa. I forgive my X and I’m ready for the next," meneja huyo wa Harmonize alisema.

Image: INSTAGRAM// KAJALA MASANJA

Mpenziwe Harmonize, Kajala Masanja amedokeza kuachana na mwanamuziki huyo na kueleza majuto yake.

Kwenye Instagram, Kajala alisema kuwa anamsamehe aliyekuwa mpenzi wake kwa yale yote alimtendea.

Hata hivyo, mama huyo hakudhibitisha ni nani haswa alikuwa anaashiria, iwapo ni Harmonize au ex wake mwingine.

"Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia,ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia😌. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala aliandika.

Alisema kuwa amekoma kufanya makosa na kurudia na ana matumaini kuwa atakuwa mtu bora kwenye maisha ya mbeleni.

Hata hivyo, Kajala hakueleza ni nini haswa kilikuwa kimetendeka mpaka kumfanya kuandika ujumbe huo.

"Hakika nimekosea familia yangu, ndugu zangu, na marafiki zangu. Kutenda kosa si kosa, kosa kurudia kosa. I forgive my X and I’m ready for the next," meneja huyo wa Harmonize alisema.

Zaidi ya hayo, Kajala alisema kuwa chapisho hilo ni la muda tu na kuna uwezekano kuwa atalifuta.

Vile vile, kwenye ukurasa wake wa Instagram, hapo awali, Kajala alikuwa amejitambulisha kama mke na meneja wa Harmonize ila sasa amefuta ujumbe huo.

Yeye na mwanamuziki huyo pia wameacha kufuatana kwenye Instagram na Kajala kuonekana bila pete yake ya uchumba.

Matendo ya hivi punde ya wawili hao haswa kwenye mitandao ya kijamii yamezua wasiwasi miongoni mwa mashabiki wao ambao wamekuwa wakihoji kuhusu kinachoendelea ndani ya uhusiano wao.