Paula Kajala ajibu madai ya kupokonywa gari na Harmonize

"Nasikia mmenyang'anywa Range," aliulizwa.

Muhtasari

• Paulah alimjibu kwa kusonya tu na kucheka ila hakufafanua iwapo ni kweli walipokonywa au ni madai tu.

• Hata hivyo, jibu lake liliashiria kuwa bado Kajala hajapokonywa gari hilo.

Paula Kajala na Fridah Kajala
Image: Kajala Instagram

Bintiye Kajala Masanja, Paulah Kajala amejibu madai ya kuwa walipokonywa gari la kifahari aina ya Range Rover na aliyekuwa mpenzi wa mama yake, Harmonize.

Gari hilo ambalo Harmonize alimzawadi Kajala kama ombi la kutaka kurudiana naye baada ya kutengana kwa mara ya kwanza ndilo lililokuwa likiashiriwa.

Kwenye video ambayo alichukuliwa, Paulah aliulizwa iwapo madai ya kupokonywa Range hio yalikuwa ya kweli.

"Nasikia mmenyang'anywa Range," aliulizwa.

Paulah alimjibu kwa kusonya tu na kucheka ila hakufafanua iwapo ni kweli walipokonywa au ni madai tu.

Hata hivyo, jibu lake liliashiria kuwa bado Kajala hajapokonywa gari hilo.

Jana Jumanne, machawa Baba Levo na Mwijaku waliwazomea Kajala na Bintiye na kusema kuwa ni watapeli.

Katika video moja ambayo Baba Levo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram wakiwa ndani ya gari na Mwijaku, wawili hao walidai kuwa Kalaja aliwakula block katika mitandao yote ya kijamii baada ya kumzomea.

Katika harakati ya kumzomea Kajala, Baba Levo alisema kuwa Kajala alitumia DM akimtusi kabla ya kumblock, huku akisisitiza kuwa arudishe magari mawili ambayo alipewa na mwanamuziki huyo wa Tanzania.

“Hapana, arudishe magari ya watu ndio nimuombe radhi. Rudisha magari kwanza ndio nikuombe radhi. Cha kwanza nimekuta meseji DM, akani’unfollow na kisha kuniblock. Yale magari arudishe,” Mwijaku alisema.

Alieleza kuwa Kajala amekuwa akimharibia Harmonize muda, jambo ambalo alitishia kufungua mashtaka.

“Nakwenda kufungua kesi ya madai mahakamani kesho . Ya kumpotezea muda msanii,” Mwijaku alisema.

Haya yamejiri baada ya Kajala kudokeza kwa mara nyingi sasa kuachana na mpenzi wake Harmonize.