"Mapenzi Tight kama kifuniko ya gesi" Diana amlisha mumewe Bahati anayeugua (Video)

Bahati ambaye hivi karibuni alifikisha umri wa miaka 30 alidhibitisha kuwa anaugua, na katika video hiyo alionekana mnyonge.

Muhtasari

• Marua aliapa kukwama na mumewe katika hali zote, wema na shari.

Diana akimlisha mumewe
Diana akimlisha mumewe
Image: Instagram

Mapenzi ya Diana Maruakwa mumewe mwanamuziki na mwanasiasa Kevin Bahati Kioko ni ya hali ya juu hata katika nyakati na hali ngumu.

Mwanablogu huyo wa YouTube alionekana kweney video akimlisha mumewe Bahati ambaye anaugua, katika video ambayo imepata umaarufu mwingi mitandaoni.

Baba huyo wa watoto watano amekuwa mgonjwa kwa siku chache zilizopita na Diana alipakia video ya kupendeza akimlisha kwenye chumba chao cha sebule. Mtayarishaji wa maudhui alimpa mumewe ugali, samaki na mboga mboga na yeye akala mlo uleule, pia.

Mwimbaji huyo wa ‘Mama’, ambaye hivi majuzi alifikisha umri wa miaka 30, alionekana mnyonge sana, lakini alifurahia chakula alipokuwa akiongea na mkewe.

Wawili hao walikuwa wakisikiliza wimbo mpya wa Diamond, Chitaki huku Marua akisema kuwa katu hatobanduka mbali na mumewe iwe kwa heri au shari.

“Katika ugonjwa na afya njema, Mapenzi Tight kama kifuniko cha gesi 😍 Hapa ni #Kavagara tuu inaongeza Raha. Upone haraka Mfalme @bahatikenya,” Diana Marua aliandika kweney video hiyo.

Mashabiki wao walimpongeza kwa kumshughulikia mumewe mgonjwa ambaye kwa kweli alionekana mgonjwa na mnyonge wa kiasi cha haja.

Mapenzi wewe 😍Muda wowote ninapotizama picha za Diana na Bahati nahisi ni kama nahitaji mwanaume na mimi mwaka 2023 lazima mume mzuri anifuate nimechoka kuangalia mapenzi ya wenyewe,” mmoja alisema.

“Lakini kusema tu ukweli nani mgonjwa hapa,  mwenye kulishana anameza kumeza hadi alisahau mgonjwa,” mwingine alitania.