Steve Ogolla amnunulia mkewe Cebbie prado TX jipya, siku 3 tu baada ya kufunga ndoa

Shemeji huyo wa Akothee alimtunuku mpenzi wake gari hilo kama mfululizo wa zawadi za kukubali kufunga ndoa ya kitamaduni naye.

Muhtasari

• Wawili hao walifunga harusi ya kitamaduni Jumatano Desemba 28 katika maeneo ya kifahari Nyanza.

Cebbie koks anunuliwa zawadi ya gari
Cebbie koks anunuliwa zawadi ya gari
Image: Instagram

Siku tatu tu tangu kufunga harusi ya kitamaduni katika sehemu moja ya kifahari maeneo ya Nyanza, mwanasheria wa mjini Steve Ogolla amepandisha viwango vya joto kwenye mapenzi yao kwa kumnunulia mke wake Cebbie Koks gari jipya aina ya Landcruiser Prado TX.

Cebbie alipakia picha na video za gari hilo jipya la rangi nyeupe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumshukuru Ogolla kwa kuendelea kumuonesha mapenzi yasiyojua kufa.

“Mtoto wangu mpya huyu hapa, ahsante sana Papi Steve Ogolla kwa zawadi hii ya ajabu mno, jipya kabisa la rangi nyeupeee KDJ,” Cebbie Koks Nyasego aliandika.

Awali Ogolla alikuwa ameweka rekodi juu kwa kulipa zaidi ya ng’ombe 30 kama mahari ambao walisindikizwa hadi kwa kina Akothee mchana peupe kila mtu akiwa ameona licha ya kashfa kutka kwa baadhi ya wanamitandao kuwa ng’ombe hao walikuwa wachanga pekee.

Ogolla alinukuliwa akisema kuwa alilazimika kufanya ihnsani hiyo bada ya kumpata Koks, mwanamke ambaye alimtaja kama mwenye mapenzi ya kweli na kukumbuka kwamba wakati mmoja aliwahi patina na mwanamke mlaghai wa mitandaoni aliyempiga zaidi ya laki tano na kumpangishia ndoa ya uongo, jambo ambalo alitaja kama lililomsababishia karibu kujitia kitanzi.

“Nilikuwa kwenye uhusiano wa uwongo na ‘mwanamke’ huyu na alinilaghai zaidi ya 500K, akapanga harusi ya uwongo na karibu kunifukuza nijiue,” Ogolla alikumbuka.

Bado inasubiriwa tamko la Akothee kumhongera mdogo wake kwa ndoa, licha ya mwanamuziki huyo awali kuweka wazi kuwa yeye na wadogo zake ni kama mafuta na maji, kwani hawawezi kupikika kwa jungu kimoja katika kile alisema kuwa ni kuonea gere mafanikio yake.