Mtoto wa Akothee, Rue Baby ampongeza Steve Ogolla kwa kuoa shangazi yake Cebbie Koks

Rue Baby alimkaribisha Ogolla katika ukoo wao na kuwahongera maharusi hao kwa hatua kubwa na kufunga mwaka wakiwa wanadoa halali.

Muhtasari

• Mpaka sasa Akothee hajatoa tamko lolote la pongezi kwa dada yake Cebbie Koks ambaye alifunga harusi ya kitamaduni Desemba 28.

Mtoto wa Akothee ampongeza Ogolla kwa kuoa shangazi yake
Mtoto wa Akothee ampongeza Ogolla kwa kuoa shangazi yake
Image: Instagram

Mtoto wa Akothee, Rue Baby amempongeza na kumshukuru mwanasheria wa mjini Steve Ogolla kwa kumuoa shangazi yake, Cebbie Koks.

Steve Ogolla Jumatano alifunga harusi ya kitamaduni na Cebbie Koks Nyasego ambaye ni mdogo wake na mwanamuziki Akothee katika hafla ambayo ilifanyika Nyanza.

Ogolla alipakia picha moja ya hafla hiyo yao kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo Rue Baby aliandika ujumbe mtamu akimkaribisha kwenye ukoo wao kwa kuoa mama yake mdogo.

“Karibu katika ukoo binamu na hongera kwa kumuoa shangazi yangu,” Rue Baby aliandika baada ya Ogolla kusema kuwa alibahatika kupata jiwe la thamani.

Tamko la Rue limechukuliwa na wengi kuwa tamko pia kwa niaba ya mama yake Akothee ambaye hakuhudhuria harusi hiyo ya dada yake mdogo.

Kwa muda mrefu, Akothee hajakuwa na maelewano mazuri na ndugu zake ambao amekuwa akiwatuhumu kwa kuonea gere mafanikio yake kimuziki na kibiashara pia.

Mwezi mmoja uliopita wakati Ogolla alimvisha pete ya uchumba Cebbie, Akothee aliweka wazi kuwa hakuwa na lengo la kuhudhuria harusi yao, jambo ambalo alilifanikisha kwa kukwepa kuhudhuria wala kuzungumzia harusi hiyo tangu Jumatano.

Lakini pia wengine wanaweza sema kuwa Akothee huenda hakufanya makusudi kukosa kuhudhuria tukio hilo kubwa la dada yake mdogo katika kile wanasema mjasiriamali huyo kwa sasa anaendelea kuomboleza kuharibikiwa na ujauzito wake – tukio ambalo limetokea siku si nyingi zilizopita.