Diamond Platnumz: Nilifikiria nitakufa wa kwanza mbele ya Costa Titch

"Yule ninamshinda miaka 5 kwelekea 6, ni mdogo sana kwa hiyo kibinadamu nilikuwa nafikiria nitatangulia kufa mimi halafu yeye anifuate." - Diamond.

Muhtasari

• Diamond alisema kwamba alitaarifiwa kuhusu kifo chake na produsa S2Kizzy lakini hakuamini mpaka alipopiga simu kwao na kusikia wanalia.

• "Mara ya mwisho nimeongoea naye kifo cha AKA juzi, ghafla naambiwa amekufa yule mdogo sana maana ana miaka 28 " - Diamond.

Diamond amuomboleza Costa Tirch, mbona hakufanya hivyo kwa AKA?
Diamond amuomboleza Costa Tirch, mbona hakufanya hivyo kwa AKA?
Image: Instagram

Kwa mara ya kwanza, msanii Diamond Platnumz amefunguka makubwa nay a ndani kuhusu ukaribu wake na msanii marehemu Costa Titch kutoka Afrika Kusini aliyefariki wikendi iliyopita akiwa jukwaani kufanya kile ambacho alikuwa anakipenda kukifanya muda wote – kutumbuiza.

Diamond amezungumza kwa upana ni kwa nini aliamua kumuomboleza Titch kwa njia ya kipekee kwa kutumia moja ya picha zake kama utambulisho wake kwenye ukurasa wake wa Instagram, jinsi alivyopokea taarifa za kifo chake na mengine ya ndani ambayo wengi hawakuwa wanajua.

Msanii huyo bosi wa WCB katika mahojiano ya kipekee ambayo yalipeperushwa kwenye kipindi cha The Switch, alionekana mnyonge huku akisema kwamab kwa wakati mmoja alihisi kwamab ni yeye angetangulia kufa mbele yam kali huyo ambaye walishirikiana katika kibao cha ‘Superstaa’

“Kwa kweli inasikitisha lakini somo kubwa ni kwamba sisi wote ni wa Mungu na kwake tutarejea kwa hiyo tujitahidi kabisa na mazingira ya kesho yetu. Mwanzo nilipoambiwa nilijua tu kadondoka chini, juu ya jukwaa kama wanavyodondoka wasanii wengine. Kumbe kafa pale pale yaani, inaonesha kwamba Mwenyezi Mungu anaweza kutuchukua muda wowote...” Diamond alisema.

Msanii huyo alisema kwamba alipata funzo kubwa kwamba anafaa kutengeneza urafiki mzuri na watu wa karibu na yeye, akiapa kuhakikisha kwamba atamaliza uhasama baina yake ya maadui wake wengi wa kimuziki.

Diamond alisema kwamba katika fikira zake, alikuwa anajua atatangulia kufa mbele ya Costa kutokana na kigezo kwamba anamzidi miaka Zaidi ya mitano.

“Kubadilisha picha yangu na kuweka picha yake, yaani maana yake msiba huu umenigusa sana. Yule alikuwa mwanangu sana halafu ananiheshimu na kunikubali sana. Mara ya mwisho nimeongoea naye kifo cha AKA juzi, ghafla naambiwa amekufa yule mdogo sana maana ana miaka 28 nimemshinda miaka Zaidi ya 5 ukienda 6. Kibinadamu nilikuwa nafikiria kwamab nitatangulia mimi halafu atafuata yeye maanake kuzaliwa nimetangulia pia..” Platnumz alizungumza kwa huzuni.

Platnumz alisema Costa alikuwa sura ya muziki wa Amapiano na mtu wa kwanza aliyemwambia taarifa zake ni produsa wake S2Kizzy na hakuamini mpaka alipopiga simu kwa familia yake na kusikia wanalia pia.