Mamake Jeff Mwathi atamani mpenzi wa mwanawe angekuwa na ujauzito wake

Kupitia TikTok, mamake Jeff alionesha ni jinsi gani alitamani mpenzi wa mwanawe Marehemu angekuwa na mtoto au hata mimba ili kuendeleza jina la Jeff.

Muhtasari

• Wengine walitamani angekuwa mjamzito ili kuhifadhi na kuendeleza jina la Jeff, tamanio ambalo Bi Mwathi alithamini sana.

Mamake Jeff Mwathi atamani mpenzi wa mwanawe angekuwa na mimba yake
Mamake Jeff Mwathi atamani mpenzi wa mwanawe angekuwa na mimba yake
Image: Screengrab, Facebook

Mamake marehemu Jeff Mwathi, Ann Mwathi, alitamani mpenzi wa mwanawe, Faith Wairimu, angekuwa mjamzito. Mama mwenye huzuni ambaye amekuwa akichapisha mara kwa mara kwenye akaunti yake ya TikTok alishiriki video yake akiwa na Faith na mume wake huku mashabiki wake wakimzonga kwa kumuonesha mapenzi binti huyo mdogo aliyekuwa mpenzi wa marehemu Jeff.

Katika video hiyo ya hivi karibuni, Faith Wairimu, mpenzi wa Jeff alionekana ameketi katikati ya wazazi wa Jeff ndani ya gari huku wimbo wa huruma ukiimba kwa mbali.

Wengine walimtaja Faith ambaye alionekana kuwa na amani na wakwe zake. Walistaajabu jinsi alivyokuwa anastarehe na wakwe zake.

Wengine walitamani angekuwa mjamzito ili kuhifadhi na kuendeleza jina la Jeff, tamanio ambalo Bi Mwathi alithamini sana.

Katika maoni ya wale ambao walisema walikuwa wanatamani Wairimu angekuwa na mimba au hata mtoto wa Jeff, kama njia moja ya kuliendeleza jina lake, mamake Jeff aliwajibu kwa kusema pia yeye alikuwa anatamani hivyo.

“Natamani ungekuwa na mimba au mtoto wa Jeff” mmoja aliandika na mamake Jeff alijibu kwa tamanio kubwa “aki!”

“Natamani sana Jeff angekuwa hata na mtoto mmoja angalau wa kuziba pengo lake,” mwingine aliandika na mamake Jeff pia akamjibu kwa jibu lile lile la kuonesha tamanio kubwa katika kauli hiyo, “aki”

Jeff Mwathi alifariki kwa njia zenye utata mwingi mnamo Februari 22 katika nyumba ya rafiki yake, DJ Fatxo mtaani Kasarani.

Kifo chake kiligubikwa na utata mwingi, baadhi wakidai huenda ni mwathirika wa visa vya ushoga vinavyozidi kuzua mjadala mkali nchini na wengine, akiwemo Fatxo wakisisitiza kwamba alijidondosha kutoka kwa roshani ya ghorofa ya 10, ambako ndio Fatxo anaishi.

Uchunguzi dhidi ya kifo chake ulikumbatiwa na DCI ambao mapema Ijumaa walitoa taarifa ya kwanza wakisema uchunguzi wa awali umekamilika.

DCI waliwataka Wakenya kuwa na subira huku wakiingia katika awamu ya pili ya uchunguzi huo na kuahidi kuwa watapekuwa kila ushahidi uliopo ili kuhakikisha Jeff anapata haki yake amabyo imekuwaq ikishinikizwa na mamia ya watumizi wa mitandao ya kijamii.