Ni vigumu kukubali kwamba kifo ni sehemu ya maisha- Viviane asema huku akimuomboleza dada yake

Vivian amefichuakuwa dadake amefariki kutokana na ugonjwa wa saratani.

Muhtasari
  • Mwimbaji huyo wa kibao cha 'chingi changa' ameshiriki msururu wa picha akiwa na dadake hospitalini
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Vivianne

Mwimbaji mashuhuri na mkufunzi wa maisha Vivian kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram alishiriki habari  za kusikitisha.

Vivian amefichuakuwa dadake amefariki kutokana na ugonjwa wa saratani.

Mwimbaji huyo wa kibao cha 'chingi changa' ameshiriki msururu wa picha akiwa na dadake hospitalini alipokuwa akipambana na ugonjwa huo.

Ni dhahiri kwamba dada yake alikuwa akipitia wakati mgumu.

"Ni vigumu kukubali kwamba kifo ni sehemu ya maisha. Dada yangu ... #CancerKills πŸ’”," mwimbaji huyo aliyevunjika moyo aliandika.

Watu kadhaa maarufu na mashabiki wametoa rambirambi zao walipomtumia ujumbe wa kutia moyo

Hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

nickmutuma:My condolences πŸ™πŸΏπŸ•Š

celestinegachuhi: My sincere condolences πŸ™

evelynwanjiru: Pole sana dear

Mavin: My condolences dear, it's not easy to lose a loved one take heart😒. May she rest in eternal peace

bossjossy254: My heartfelt condolences @vivianne_ke

njorogemeri: My Condolesence ,may her soul rest in peace πŸ•ŠπŸ•Š

carbella_trends: Sorry dear.....one day cancer will also die😒