Mwimbaji wa Jamaica, Konshens akubali jina lake la Kenya 'Otieno'

Kwenye remix ya wimbo 'Anjella' alionekana kulikubali jina hilo kwa moyo mkunjufu.

Muhtasari

•Upendo mkubwa wa mwimbaji huyo kwa Kenya uliwafanya watumiaji wa mitandao ya kijamii wabunifu kumpa jina Konshens Otieno.

•Kwenye kitambulisho alichotengewa na Mkenya mbunifu, msanii huyo mzaliwa wa Jamaika alisemekana kuzaliwa Kisumu, Kenya.

Konshens
Image: HISANI

Staa wa nyimbo za Dancehall Garfield Delano Spence almaarufu Konshens amekubali jina la majazi ambalo alibandikwa na Wakenya kufuatia uhusiano na upendo wake mkubwa kwa taifa hili.

Upendo mkubwa wa mwimbaji huyo kwa Kenya uliwafanya watumiaji wa mitandao ya kijamii wabunifu kumpa jina Konshens Otieno na Mkenya mmoja hata akamtengenezea kitambulisho cha Kenya.

Konshens kwenye remix yake na rapa Boutross Munene ya wimbo maarufu 'Anjella' alionekana kulikubali jina hilo kwa moyo mkunjufu.

"Brace  pan di wall and fling it up gimmi nuh,

Konshens AKA Otieno,

Play with the two ni++le like Piano," Konshens aliimba.

Kwenye kitambulisho alichotengewa na Mkenya mbunifu, msanii huyo mzaliwa wa Jamaika alisemekana kuzaliwa Kisumu, Kenya.

Mapema mwaka jana baada ya tamasha lake la kusisimua humu nchini Kenya, pia alionekana kukubali jina hilo alilopewa huku akiwaaga Wakenya. Wakati huo, aliahidi kurudi baada ya miaka michache.

"Upendo mkubwa Kenya, imekuwa ya kweli, muungano wetu una nguvu kuliko awali. Tutaonana tena baada ya miaka 3/4 Konshensn Otieno," aliandika kwenye Twitter na kuambatanisha na emoji ya bendera ya Kenya.

 

Upendo wa mwimbaji huyo wa Dancehall na Reggea kwa Kenya ni dhahiri na amethibitisha hilo kwa ziara zake kadhaa. Konshens ni mgeni wa mara kwa mara nchini Kenya na ziara yake ya mwisho ilikuwa Desemba 2021.

Wakenya wengi pia wanamshabikia Mjamaica huyo na hata kumfuatilia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.