Usiseme unataka kuwa msanii-Nadia amwambia mwanawe huku akishereheea siku yae ya kuzaliwa

Aliendelea kufichua kuwa mwanawe ana shughuli nyingi na mzungumzaji kama yeye.

Muhtasari
  • Nadia alimwandikia mwanawe ujumbe mtamu, akisema kwamba amekuwa na ndoto ya kupata mtoto wa kiume na Mungu alimbariki na mmoja.
Arrow Boy, Nadia Mukami na mtoto wao Kai
Image: Nadia Mukami Instagram

Mkurugenzi Mtendaji wa Utembe World Arrow Bwoy na mchumba wake Nadia Mukami kwa mara ya kwanza wamefichua sura ya mwana wao Kai baada ya mwaka mmoja.

Ufunuo huo ulifanyika siku ya Ijumaa, wakati KAI alikuwa anatimiza mwaka mmoja.

Nadia alimwandikia mwanawe ujumbe mtamu, akisema kwamba amekuwa na ndoto ya kupata mtoto wa kiume na Mungu alimbariki na mmoja.

Aliendelea kufichua kuwa mwanawe ana shughuli nyingi na mzungumzaji kama yeye.

“Mtoto anafanana na nani? …Sikuzote nilitaka mtoto wa kiume vibaya sana na Mungu alinijalia mtoto @haseebkai Wewe ni kama mama mwenye bidii na mzungumzaji 😁 Umenipa sababu mpya ya kuhangaika zaidi!

“Naomba kesho ungependa kuwa msanii☹️🙄😁😁 tafadhali kuwa wakili wa familia yetu 😁😁😂 Happy Birthday @haseebkai,” Nadia Mukami alimsherehekea mwanawe.

Kwa upande mwingine, Arrow Bwoy pia alimsherehekea mwanawe kwa ujumbe uliosomeka;

“Heri ya siku ya kuzaliwa mwanangu @haseebkai Mola wetu amekuwa Mwendeshaji wa kasi na napenda kasi Alhamdulilah 🙏🏾❤️❤️❤️ Kaende sana 😁 . @mutemwa 🔥🔥🔥📸,”.

Nadia Mukami na Arrow walikaribisha baraka yao ya furaha mnamo Machi 24, 2022.