Sitaki awachane na mchumba wake - Pritty Vishy asema sababu ya kutopakia mpenzi wake

Hata hivyo, Vishy alipakia picha ambayo ilionesha tattoo ya jina la mpenzi wake mpya kwenye kidole chake cha pete.

Muhtasari

• Awali kulikuwa na picha iliyokuwa ikienezwa mitandaoni kuwa Vishy alichora tattoo ya mpenzi wake huyo mpya kwenye kidole chake cha pete.

Pritty Vishy atoa sababu ya kutomuonyesha mpenzi mpya
Pritty Vishy atoa sababu ya kutomuonyesha mpenzi mpya
Image: Instagram

Mwanablogu Pritty Vishy amedokeza kwamba hatimaye amepata mpenzi mpya ila akasema kwamba hayuko tayari kabisa kumuonesha kwa wafuasi wake mitandaoni.

Vishy alikuwa anashiriki kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram yake ambapo mmoja alitaka kujua ni lini anatarajia kuwaonesha wafuasi wake sura ya mpenzi wake mpya.

Mwanablogu huyo alisema kuwa hayuko tayari kumuonesha akitetea uamuzi wake kwamba mpenzi huyo wake ana mpenzi mwingine na hivyo wanawake wawili wako katika maisha yake.

Alisema kwamba hataki kumuonesha mitandaoni kwa sababu hataki aachwe na mpenzi wake mwingine.

“Sina uhakika wa kumpakia wakati wowote hivi karibuni kwa sababu ana mpenzi mwingine. Sitaki awachane na mchumba wake,” Vishy alisema.

Awali kulikuwa na picha iliyokuwa ikienezwa mitandaoni kuwa Vishy alichora tattoo ya mpenzi wake huyo mpya kwenye kidole chake cha pete.

Wiki jana, Vishy alisema kuwa anaishi kwa wasiwasi mkubwa kutokana na watu asiowafahamu kumtafuta kwa njia ya WhatsApp na simu wakimtaka kujumuika nao katika kufanya ajira ya kuigiza filamu za michezo ya watu wazima.

Katika picha ya mazungumzo yao kupitia WhatsApp, watu hao walikuwa wamemuahidi kiasi cha shilingi laki 6 endapo angekubali kushiriki katika filamu hizo, wakisema kwamba walivutiwa na yeye kwani walikuwa wanataka mtu mwenye mwili wa kibonge kama yeye.

Hata hivyo, Vishy alikataa kukubali ofa hiyo, akisema kwamba ametosheka na kile kidogo anachokipata kwani kwake kushiriki katika kuigiza video za watu wazima ni kuichoma picha yake kwa jamii inayomuangalia kama kielelezo cha maadili mema.