Nyoro ajawa na furaha baada ya Yesu wa Tongaren kum'follow kwenye Facebook

"Huyo anatafuta wale wezi wawili wa kusulubisha na yeye, Nyoro kaa chonjo," mmoja alimtaadharisha.

Muhtasari

• Hata hivyo, baadhi walizua utani wakisema huenda huyo si Yesu wa Tongaren halali.

• Wengine walisema kuwa amepakwa mafuta kuwa mmoja wa watu 2 wa kwenda mbinguni kutoka Nairobi.

Ndungu Nyoro afurahia kufuatwa Facebook na Yesu wa Tongaren.
Ndungu Nyoro afurahia kufuatwa Facebook na Yesu wa Tongaren.
Image: Facebook, Maktaba

Ndungu Nyoro ni mtu mwenye furaha baada ya kudai kwamba mhubiri anayejitambulisha kama Yesu wa Tongaren kutoka kaunti ya Bungoma kuanza kumfuata kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Nyoro ambaye mwanaharakati wa kufadhili elimu ya watoto wasiokuwa na uwezo kutoka kundi la Affecto, alipakia picha ya skrini ya Facebook yake akionesha upande wa taarifa za watu wapya ambao wamemfuata katika uurasa wake kwenye mtandao huo maarufu.

Mmoja wa wale ambao waliamua kumfollow Nyoro ni jamaa kwa jina la Yesu wa Tongaren, haijulikani kama ni akaunti halali ya mchungaji huyo mwenye utata au ni akaunti ghushi tu ya mtu ambaye anajaribu kuteleza kwa ganda la ndizi kwa umaarufu wa ‘Yesu’.

“Sasa ona nani huyo ameamua kumfollow mtoto wa WaNdungu,” Nyoro aliandika kwenye ukurasa wake kwa furaha.

Baadhi ya wafuasi wake walizua utani wakimtahadharisha kuchunga asije akasulubishwa na yeye msimu huu wa pasaka – haswa baada ya madai kuibuka kwamba kuna vijana ambao wamemweka chini ya shinikizo Yesu huyo wakimtaka kujitokeza na kusulubishwa wakati wa pasaka, kama anaamini kabisa yeye ni Yesu wa ukweli, kwani hafai kuogopa maana baada ya siku tatu atafufuka.

“Kati ya watu wawili wa Nairobi wanaokwenda mbinguni wewe ni kati ya wawili au kati ya watu wawili waliosulubiwa naye Pasaka iko karibu!” mmoja alimwambia.

“Chunga usisulubishwe na yeye,” mwingine akatania.

“Anatufuta wezi wawili ambao watasulubishwa na yeye, Nyoro kuwa macho,” huyu naye alimtaadharisha.