Amber Ray afichua kwa nini anafanyiwa masaji ya ujuzito kwenye tumbo

Mwanamitindo huyo alisema kuwa zimebaki siku 10 tu kuelekea hafla ya baby shower.

Muhtasari

• Hivi majuzi Amber Ray alidai kuwa walitengana na mpenzi wake Kennedy Rapudo ambaye walikuwa wamechumbiana kwa miezi kadhaa.

• Alidai kuwa alikuwa amechoka na mapenzi.

Amber Ray atoa onyo kali dhidi ya ex wanaomchafulia jina baada ya kuachana.
Amber Ray atoa onyo kali dhidi ya ex wanaomchafulia jina baada ya kuachana.
Image: Instagram

Mwanasosholaiti maarufu Amber Ray amefichua siku zilizobaki afanye karamu ya 'Baby Shower' ya mwana anayemtarajia.

"Imebaki siku 10 ili nifanye babyshower, siwezi tulia ,umealikwa lakini?' alisema Amber Ray.

Mama huyo wa mvulana mmoja pia aliwaonyesha mashabiki akienda kukandwa ujauzito wake huku akisema lazima mtoto wake azoee maisha ya raha mapema.

"Leo ni kukandwa,mtoto lazima azoee maisha ya raha mapema." alidokeza Ray.

Amber Ray hapo awali alikuwa ameandaa karamu ya kufichua jinsia ya mtoto wake iliyoleta vita ya mtandao kati yake na mwanasosholaiti Vera Sidika aliyedai kuwa Ray alinakili maudhui yake ya karamu ya kufichua jinsia ikiwemo kutumia chopa na kumwagiwa pesa.

 

Hivi majuzi Amber Ray alidai kuwa walitengana na mpenzi wake Kenny Rapudo ambaye walikuwa wamechumbiana kwa miezi kadhaa.Alidai kuwa alikuwa amechoka na mapenzi.

Kwa upande wake, Rapudo alidai kuwa ukweli utadhihirika hivi karibuni ili kutathmini chanzo cha kutengana kwao. Rapudo alipuzilia mbali madai kuwa ujauzito wa Ray sio wake akithibitisha kuwa mtoto ni wake na atamshughilikia.

Rapudo alimvisha mwanasoshalaiti huyo pete ya uchumba mwishoni mwa mwaka jana jijini Dubai ambako walikuwa wameenda likizo.

Wawili hao waliingia kwenye mahusiano ya kimapenzi katikati mwa mwaka jana baada ya kuwa marafiki kwa muda.