Rapa Tekashi 6ix9ine ku'shoot video Afrika akitumia simu ya Iphone

Tekashi alifurahishwa na video ya watoto wakicheza wimbo wake mpya wa Wapa, ambao alisema video ataifanya Afrika.

Muhtasari

• Tekashi aliwashauri wasanii wanaoanza kutojali wala kuhangaika katika masuala ya video.

• Alisema kuwa video nzuri pia inaweza ikafanyika kwa kutumia simu ya Iphone bila kugharamika kwingi.

Msanii 6ix9ine kufanya video ya Wapa Afrika kwa kutumia Iphone.
Msanii 6ix9ine kufanya video ya Wapa Afrika kwa kutumia Iphone.
Image: Instagram

Tekashi 6ix9ine, rapa kutoka Marekani ametangaza kufanya mradi wake wa video ya ngoma mpya katika bara la Afrika.

Rapa huyo ambaye alishambuliwa na wahumi wii mbili zilizopita akiwa kwenye gym huko Florida Marekani kupitia Instagram yake alipakia video ya watoto wakicheza ngoma yake na kusema kuwa video hiyo imempa motisha na uchu wa kutaka kufanya video rasmi ya wimbo huo katika bara la Afrika.

Hata hivyo, Tekashi hakuweka wazi ni taifa gani atafanya video yake, akiwataka mashabiki wake kumtajia mataifa ambayo wangependa kumuona akifanya video yake.

Msanii huyo alisema kuwa katika ziara yake Afrika, hatoongozana na timu yake ya kufanya video bali atabeba tu simu yake aina ya Iphone na kuitumia katika kufanay video hiyo.

“Niko njiani kuelekea Afrika kurekodi video ya muziki bila timu ya kamera. Tarehe 10 Aprili ni leo … nilikuahidi video ya muziki siku 3 kuanzia sasa tarehe 14. Kiuhalisia sitafanya tarehe hiyo LAKINI mara tu nitakapoanza kurekodi sitaacha na kukupa tarehe yoyote nitakayomaliza,” Tekashi alisema.

Msanii huyo alisema kuwa kufanya video na simu haimaanishi kwamba amefilisika au lebo yake haimuungi mkono au hata kutokuwa na kamera, alisema ana kamera nzuri tu ya Sony lakini chaguo lake la kufanya kamera kwa simu ni la kipekee kwani angependa kutangamana na watu wengi katika sehemu mbali mbali Afrika.

“Tunaelekea uwanja wa ndege na hiki ni kitu cha ajabu sana tutaenda kukifanya. Tuko na kamera rasmi ya kufanya kazi ya Sony lakini tulinunua simu hii katika duka la Best Buy na mtaona video ya wimbo mpya wa Wapa ikishootiwa kwenye simu ya Iphone,” alisema.

Pia aliwashauri wanamuziki chipukizi na wale walioko chini la lebo ambao wanateta kuwa lebo haziwafanyii kazi, akisema kuwa hivyo ni visingizio tu kwani video nzuri inaweza pia ikafanywa kwa simu ya Iphone tu bila kuchakarika kwingi.