Fahamu kwa nini Samidoh anavuma Twitter

Kwa miaka mingi, watu mashuhuri wengi wamehusika katika kashfa za nje ya ndoa, na kuwaacha mashabiki wao vinywa wazi.

Muhtasari
  • Mwanamuziki huyo wa Kikuyu ni mwanamume mwenye ndoa yenye furaha, na uhusiano wake na Karen umeacha ndimi zikiyumba.
Nyamu asema Samidoh huwa anamuomba kofia yake.
Nyamu asema Samidoh huwa anamuomba kofia yake.
Image: Insatgram

Mwimbaji wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh anavuma tena, baada ya mwanablogu maarufu Edgar Obare kushiriki video yake na ‘mwanamke mwingine.

Kulingana na video hiyo mpya ambayo imesambaa kwenye mtandao wa Twitter, Samidoh anaonekana akiburudika ndani ya gari na mwanamke huyo ambaye hajatambulika.

Kwa miaka mingi, watu mashuhuri wengi wamehusika katika kashfa za nje ya ndoa, na kuwaacha mashabiki wao vinywa wazi.

Uhusiano wa Samidoh na mkewe Eddah na Karen Nyamu ni wa ajabu sana wenye misukosuko na zamu.

Uchumba wake nje ya ndoa na Nyamu umekuwa ukienea kwenye vyombo vya habari katika miaka michache iliyopita.

Mwanamuziki huyo wa Kikuyu ni mwanamume mwenye ndoa yenye furaha, na uhusiano wake na Karen umeacha ndimi zikiyumba.

Wanamitandao waita maoni tofauti kuhusu video hiyo na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

TheOneEdd: Are you sure Samidoh is kikuyu? Ehhh

Nam_saying: what time does he maintain law and order?

ibrualle: Wacha achaje wafuasi.. kwani iko nene

cathy_mutuku: Tafuta pesa mapenzi inajileta, senator about to leave the country

karennyamunbo: atapata another pg soon to make this side chic jealous

GeorgeKayman76: Samidoh is a lower version of Akothee