Davido amjibu mwanahabari aliyetaka kujua kwa nini hazungumzii kifo cha mwanawe

Mwanahabari huyo aliuliza ni kwa nini albamu yake inaonekana yenye furaha na sherehe na haioneshi huzuni wowote kwa kufiwa na mwanawe.

Muhtasari

• Hata hivyo Davido alisema kuwa albamu yake ngoma nyingi ziliandikwa kabla ya kifo cha mwanawe.

•Aliahidi kuwa endapo kuna muda atalazimika kulizungumzia basi haitakuwa kupitia wimbo bali kwa njia nyingine tofauti.

Davido hatimaye aachia albamu yake mpya "Timeless"
Davido hatimaye aachia albamu yake mpya "Timeless"
Image: Twitter

Msanii wa Nigeria, Davido alitoa majibu ya ukomavu kwa mmwanahabari aliyeuliza kwa nini hakuandika wimbo wowote kuhusu kifo cha mwanawe kwenye albamu yake ya hivi karibuni kama baba mwenye huzuni.

Katika mkutano na wanahabari kuhutubia kuhusu albamu yake mpya iliyotolewa hivi karibuni ya Timeless, mtangazaji huyo alilalamika kwamba albamu hiyo ilikuwa ya "sherehe" sana, wakati wengi walikuwa wanamtarajia kuonesha huzuni.

"Wimbo huu ni wa sherehe sana, unapaswa kuweka huzuni ndani yake baada ya kile tunachojua kilitokea. Namaanisha, hakukuwa na kutajwa au kumbukumbu ya mwanao na watu wanasema hawaelewi, kwa nini?" aliuliza.

Albamu hiyo ilitolewa miezi sita tu baada ya Davido kupoteza mwanawe wa kwanza, Ifeanyi, na mtoto pekee na mkewe, Chioma Rowland Adeleke.

Wakati mwanahabari huyo akiuliza swali hilo, meneja wa Davido, alijaribu kumzuia kwa sababu ilionekana kutokuwa na hisia na sio lazima.

Lakini Davido alieleza kwa uzuri kwamba, nyimbo nyingi kwenye albamu yake zilirekodiwa kabla ya kifo cha Ifeanyi.

Kulingana naye, ana mpango wa miradi yake yote na albamu ya 'Timeless' inakusudiwa kuwa albamu ya kawaida, bila kujali alikuwa akipitia nini.

“Maisha yangu yamegawanyika na muziki wangu. Kama mwanamuziki, nilitaka kutoa albamu ya kawaida. Ukisikiliza nyimbo zangu kwa mwaka mzima, utajua Davido ni mtu mwenye furaha hivyo albamu hii haina tofauti. Kuna hisia, ndio, lakini wakati sahihi utakuja kuutumia kwa wimbo. Siku zote nimekuwa mtu mwenye furaha iwe ninapitia jambo fulani au la. Kwa hivyo upande huo wa maisha yangu, ikiwa nataka kuongelea, kuna wakati wa hilo, lakini kwa albamu hii, hiyo haikuwa kile nilichokuwa nataka kuzungumzia," Davido aliongeza.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Lagos Nigeria, Davido aliahidi kwamba tamasha la 'A Timeless Night' litakuwa tukio la kusisimua.

Akiwahutubia waandishi wa habari, Davido aliwahakikishia mashabiki kuwa amemtembelea Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Lagos ambaye aliahidi kutoa ulinzi wa ziada kwenye eneo la tamasha hilo.