Kwa mara ya kwanza Rayvanny ampokonya Diamond nafasi ya kwanza kwa kishindo

Rose Muhando anasalia kuwa msanii pekee wa injili ambaye anajinafasi katikati mwa kundi la wasanii wa sekula, akiwa ametazamwa mara milioni 5.9 ndani ya mwezi Aprili pekee.

Muhtasari

• Rayvanny alitazamwa mara milioni 40 huku Diamond aliwa na utazamwaji mara milioni 35.

• Hata hivyo, baadhi walihisi mchezo mchafu wakidai kuwa Rayvanny hangeweza kumpiku Diamond.

Diamond na Rayvanny
Diamond na Rayvanny
Image: Instagram

Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka mingi, Msanii Rayvanny kutoka lebo ya Next Level Music amemdungua aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz kutoka nafasi ya kwanza kweney chati za wasanii waliotazamwa Zaidi kwa mwezi.

Kwa muda mrefu, Diamond amekuwa akiongoza kweney chati za muziki kila mwezi ukanda wa Afrika Mashariki, hata wakati ambapo hajatoa miziki mipya.

Lakini safari hii historia imeandikwa. Kwa mujibu wa Charts Tanzania, Rayvanny amekuwa msanii wa kwanza kufanikiwa kumtoa Diamond katika kilele cha chati hizo kwa kishindo na kuibuka kidedea kuwa msanii aliyetazamwa Zaidi YouTube katika mwezi uliopita wa Aprili.

Imekuwa Zaidi Ya Miaka Mingi Diamond Platnumz Amekuwa Akiongoza List Ya Wanamuziki Wa Tanzania Wanaotazamwa Zaidi YouTube Kwa Kila Muhula Ila Mwezi April 2023 Rais Wa Next Level @Rayvanny Amefanikiwa Kuvunja Rekodi Hiyo Na Kuwa No 1 Ya Wanamuziki Wa Tanzania Waliotazamwa Zaidi YouTube April 2023,” Charts Tz walimhongera Chui.

Katika orodha hiyo, Rayvanny alitazamwa mara milioni 40 kwenye YouTube huku bosi wake wa zamani Diamond akiibuka wa pili kwa mbaali akiwa na utazamwaji wa milioni 35.

Mbaya wake Harmonize aliibuka wa tatu akiwa na utazamwaji wa milioni 22 naye Zuchu akifunga nne bora kwa watazamaji milioni 12 ndani ya mwezi Aprili pekee.

Hao ndio wasanii wane amabo walipata utazamwaji wa Zaidi ya milioni 10 kwenda mbele ndani ya siku 30 zilizopita.

Kwa mara nyingine tena, msanii Rose Muhando alisalia kuwa wa pekee kutoka Sanaa ya injili ambaye alijinafasi katika orodha ya kumi bora, akishikilia nafasi ya nane na utazamwaji wa milioni 5.9 katika mwezi wa Aprili.