Nimekataliwa mara mingi-Justina Syokau afichua sababu ya kuwa singo

Justina alifichua kwamba anampenda Akothee kwa ajili ana bidii, licha ya kuwa 'single mother'.

Muhtasari
  • Msanii huyo alisema kwamba baadhi ya wanawake ambao wanawalea watoto peke yao hawakuchagua njia hiyo ilhali walijipata tu.
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Image: HISANI

Msanii wa nyimbo za injili Justina Syokau hatimaye amefichua sababu ya kuwa mseja kwa zaidi ya miaka 5.

Akiwa kwenye mahojiano na Mungai Eve siku ya Jumatatu mama huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba wanaume wengi wamekuwa waimuacha baada ya kuwaambia kwamba ana mtoto.

"Mi nina mtoto mmoja na nina miaka kumi hapa nje pekee yangu. Unakuta tukipatana na watu pale nje watu wanakataa mtoto tu mmoja."

 

Kulingana na Syokau amekataliwa mara nyingi kwa sababu ana mtoto.

"Nimekataliwa mara mingi. Wakati unaambia mwanaume uko na mtoto anaona ni burden. Unakuta alikuwa na appetite ya kuwa na wewe, alikua na mpango anataka kukuoa. The moment unamwambia wewe ni single mother uko na mtoto unaona ameboeka.

Msanii huyo alisema kwamba baadhi ya wanawake ambao wanawalea watoto peke yao hawakuchagua njia hiyo ilhali walijipata tu.

"So kuwa na mtoto si kuwa na maisha mabaya. At least mimi nilikuwa nimeolewa. Kuna wasichana mtu alipata mimba class eight na amesoma hadi university, huwezi kataa msichana yule juu hajia olewa.

Justina alifichua kwamba anampenda Akothee kwa ajili ana bidii, licha ya kuwa 'single mother'.

   "She has been president of single mothers na mimi ni single mother. Anaeza kuwa hajaokoka lakini Akothee nampenda juu ako na bidii,"Alisema.

Miezi 3 iliyopita Syokau alirudi kwa kishindo kikuuu kwenye mitandao ya kijamii huku akionyesha safari ya maendele ya muonekano wake mpya.

Syokau alipakia picha akiwa na muonekano tofauti kabisa, umbile la kishua ambalo alisema kuwa ana furaha isiyoweza kumithilika kwa umbo la mwili wake jipya.

“Hatimaye nimefanikisha lengo langu la kupata makalio makubwa. Napenda muonekano wa mwili wangu mpya,” Syokau aliandika Instagram.

Haijulikani kama alifanya upasuaji wa kuongeza makalio ama ni uhariri wa picha ambao alifanya ili kuonekana na makalio makubwa ya kipekee.

Aidha, alisema kuwa kuongeza makalio yake hakutakuwa kwa kuwapendeza na kuwavutia wanaume bali tu kama njia moja ya kutumia muonekano wa mwili wake mzuri kuzidi kusambaza injili ya Mungu.

"Nataka kutengeneza mwili wangu, hata natafuta milioni 3. Yaani si ukiumwa na jino huwa unaenda hospitalini kung'olewa jino hilo? Sasa mimi nataka kutolewa mafuta kwenye mwili wangu ili yawekwe mahali inayostahili, kwa utukufu wa Mungu," Justina alieleza sababu yake.

"Nataka kutoa mafuta kwa tumbo, kwa mapaja na kwa mgongo ili yote yapelekwe mahali pamoja ambapo ni makalio. Watu wanasema kuwa hawataki lile umbo la Vera ila mimi nalitaka, lile umbo ni zuri, bora ulitumie kwa utukufu wa Mungu," aliongeza.