Mpenzi wa zamani wa Diamond, Hamisa Mobetto amtambulisha mpenzi mpya

Wiki tatu zilizopita katika mahojiano, Mobetto alisema umri unazidi kumpa kisogo na anatamani sana kupata mume na kutulia katika ndoa.

Muhtasari

• Mobetto alipakia picha ya mpenzi huyo mpya kwenye instastory na kuisindikiza na emoji ya mahaba.

Hamisa Mobetto akizungumza kuhusu kutamani ndoa.
Hamisa Mobetto akizungumza kuhusu kutamani ndoa.
Image: Screengrab// YouTube

Hamisa Mobetto amekuwa gumzo la mitandaoni baada ya kuoneshana makopakopa hadharani na afisa wa mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe.

Mambo yalichemka mitandaoni Jumatano baada ya Hamisa ambaye muda mwingi si mpakiaji wa mara kwa mara mitandaoni alipopakia picha ya Ali Kamwe kwenye instastory yake na kuisindikiza na emoji ya mahaba.

Hamisa kwa wale wanaomjua kwa miaka mingi tu iliyopita, hajawahi kumpakia mwanamume yeyote kwenye Instagram yake kando na kupakia biashara zake ikiwemo ni zile za biashara za nguo lakini pia na matangazo ya ubalozi wa kampuni ya kucheza Kamari.

Kwa upande wake, Ali Kamwe naye hakuachwa nyuma. Kocha huyo pia alipakia picha ya Mobetto kwenye instastory yake na kuandika ‘rahaa’ – jambo ambao lilichemsha mitandao ya kijamii wengi wakisema kuwa si kawaida wawili hao watakuwa na jambo lao.

Wengi wanaamini kwamba wawili hao watakuwa wameotesha huba zito baina yao kwani haiwezekani kuwa ni kiki sababu mmoja ni msanii – Hamisa na mwingine ni mtu ambaye masuala yake yako mbali kabisa na biashara ya usanii unaohitaji kiki – Ali Kamwe.

Wiki chache zilizopita katika mahojiano na Millard Ayo, Mobetto alinukuliwa akisema kwamba katika siku za hivi karibuni, amekuwa akitamani sana kupata mwanamume wa kumuoa na angalau kuwazawadi wazazi wake na mkwe.

Mama huyo wa watoto wawili alisema kuwa miaka ya nyuma hakuwa anaona umuhimu katika ndoa lakini katika siku za hivi karibuni kadri umri unavyozidi kumpa kisogo, amekuwa akitamani sana kuolewa ila akasema kuwa hawezi akaolewa na mwanamume ambaye yeye anamzidi kipato.

Alisisitiza kwamba anataka mwanamume mwenye pesa zake na yeye kazi yake itakuwa kumkuzia familia tu basi!

Hamisa Mobetto alianza kujulikana baad ya kutoka kimapenzi na msanii Diamond Platnumz na mwaka jana alisemekana kutoka kimapenzi na Rick Ross japo alikanusha na kusema tu ni washikaji.